Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 4, 2017

Chama cha Waziri mkuu wa Japan chashindwa katika uchaguzi Tokyo

Chama cha Liberal Democratic Party, LDP, kilishindwa katika uchaguzi wa manispaa uliofanyika mjini Tokyo Jumapili.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, Jumatatu aliahidi kufanya kila juhudi ili kupata tena imani ya Wajapan baada ya chama chake cha Liberal Democratic Party, LDP, kushindwa katika uchaguzi wa manispaa uliofanyika mjini Tokyo Jumapili.
Chama hicho kilitarajiwa kupata viti 23 katika bunge hilo jipya, ambapo kimeshuka sana kutoka kwa idadi ya viti 53 kilivyokuwa navyo hapo awali. Gavana wa Tokyo Yuriko Koikie na chama chake cha Citizens First Party, pamoja na washirika wake, watashinda angalau viti 72 kwenye bunge hilo litakalokuwa na jumla ya viti 127.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba uchaguzi huo wa Tokyo haukumhusu sana Koikie, bali ni kama kura ya maoni kuhusu Waziri mkuu Abe, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kumsaidia rafiki yake kupata idhini ya kujenga taasisi ya masomo kuhusu tiba ya wanyama, katika eneo maalum la Kiuchumi, jambo amalo ni nadra kufanyawa katika serikali ya Japan.
Abe hata hivyo, amekanusha shutuma hizo, ambazo zimeshusha umaarufu wake.

VOA Swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment