Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 19, 2017

Caf yafikiria kubadili tarehe ya kuandaa kombe la taifa bingwa Afrika

Kombe la taifa bingwa barani Afrika huenda likahamishwa hadi msimu wa joto kama sehemu ya mazungumzo ya shirikisho la kandanda barani Afrika.

Kuandaliwa mashindano hayo miezi ya Januari na Februari imeghadhabisha vilabu vya bara Ulaya ambapo wachezaji wengi wa kiafrika hucheza.

Pia idadi ya timu zinashoriki huenda ikaongezwa kutoka 16 hadi 24.

Wachezaji wengine walikataa ombia la kuwataka kujiunga nchi zao kushirikia mashindani ya mwaka huu, yaliyoandaliwa nchini Gabon na kuamua kubaki na vilabu vyao.

Hao ni pamoja na wachezaji kadha kutoka Cameroon ambao walitaka kujiunga na timu ambayo hata hivyo ilishinda kombe hilo.

Kila baada ya miaka miwoli mzo huibuka kati ya vilabu vya Ulaya na nchi, vinavyodai kuwapoteza wachezaji wakati wanahitaji sana.

Kwa mujibu wa vilabu hivyo mara nyingi wachezaji hurudi vilabuni wakati wamechoka baada ya kuishiriki mechi za taifa bingwa barani Afrika.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment