Wanamgambo wa Boko Haram waripotiwa kutekeleza mashambulizi mawili ya bomu kaskazini Mashariki mwa Cameroon na kupelekea vifo ya watu 14 huku 40 wakijeruhiwa .
Mabomu hayo yalitegwa eneo la soko lenye shughuli nyingi linalojulikana kama Waza mpakani mwa Nigeria .
Mbali na kusababisha vifo na kujeruhi watu, mabomu hayo yamepelekea hasara katika vibanda vya biashara, nyanya za umeme na simu kuharibiwa .
Taarifa za hivi punde zafahamisha kwamba mji huo umefungwa kwa muda hamna mtu yeyote atakayeruhusiwa kuingia wala kutoka.
Ingawaje kundi haramu la Boko Haramu limeundiwa Nigeria, wanamgambo hao wamekuwa wakiendeleza mashambulizi kati nchi jirani za Cameroon, Niger na Chad.
No comments
Post a Comment