UWANJA WA JAMHURI DODOMA.
ZIKIWA zimesalia siku chache kuchezwa kwa fainali ya mashindano ya Kombe la FA, uwanja wa Jamhuri mkoani hapa umezidi kuimarika kwa nyasi zilizopandwa kuota vizuri, imeelezwa.
Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa Mei 28, mwaka huu kwa kuzikutanisha Simba ya jijini Dar es Salaam dhidi ya Mbao FC na mshindi atakata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja wa uwanja huo, Antony Nyembela, alisema mchakato wa kumwagia maji na kupanda nyasi katika maeneo yaliyokuwa yameharibika unaendelea vizuri na kwamba uwanja huo kwa sasa unaonekane kuwa mpya.
"Tangu tulipoambiwa sisi ni wenyeji wa fainali hiyo, tumekuwa na matengenezo, tumepanda nyasi katika maeneo yaliyokuwa na vipara na tunamwagilia maji kila siku, ninaamini hadi siku ya mechi vipara vyote baadhi ya maeneo ya uwanja vitakuwa vimeisha," alisema Nyembela.
Kuhusiana na mashabiki, aliwatoa hofu kwa kuwaambia ulinzi utapatikana huku akisema kuwa uwanja huo una uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 15,000 baada ya kufanya tathmini kwa kuwashirikisha wamiliki ambao ni Chama cha Mapinduzi.
No comments
Post a Comment