Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 8, 2017

Viongozi wa TRA watafikishwa mahakamani kwa kuliingizia taifa hasara



Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola

BAADHI ya viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), watafikishwa mahakamani kutokana na kuliingizia taifa hasara iliyotokana na rushwa kwa kuwa na uhusiano na mfanyabiashara anayetuhumiwa kuliibia taifa Sh milioni saba kila dakika.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola aliyasema hayo mjini hapa kwenye semina ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika Wanaopambana na Rushwa (APNAC) tawi la Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu huyo alisema waandaamizi hao wanatafikishwa mahakamani kutokana na makosa ya rushwa yanayowakabili.

Alisema viongozi hao, watafikishwa mahakamani baada ya kugundulika kushirikiana na wafanyabiashara wajanja wachache kuiibia serikali na kulikosesha taifa mapato.

“Viongozi hawa watafikishwa mahakamani baada ya kubainika kushirikiana na mshitakiwa mmoja aliyopo mahakamani kwa sasa kujipatia Sh milioni saba kila baada dakika…huyo mshitakiwa hakuweza kufanya wizi huo pekee yake, lazima alishirikiana na viongozi wa TRA maana ‘link’ ya wizi wa mtambo wake wa kutoa stakabadhi uliunganishwa na ule wa serikali,” alisema.

Hata hivyo, alisema Polisi wamekuwa magwiji wakubwa wa kupokea rushwa, hivyo kuonekana kuwapo na mifumo dhaifu ya kuweza kukabiliana na tatizo hilo.

“Kila sehemu kuna rushwa, kuanzia suala la ugaidi ambapo watuhumiwa hupitisha silaha zao mipakani na kuwapa rushwa wahusika, dawa za kulevya wanatoa nchi za mbali na kufikishwa nchini…kila sehemu tatizo ni hilo,” alisema.

Vilevile, alisema tatizo la rushwa nchini bado kubwa, hivyo wabunge wanatakiwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wanalipigia kelele kila wanapokuwa katika maeneo yao ya kuwatumikia wananchi.

Aidha, alisema lazima Rais awe na dhamira mahususi ya kupambana na rushwa kama anavyofanya sasa pamoja na utawala bora ili kuweza kusaidia kukabiliana na tatizo hilo.

Mwenyekiti wa mtandao huo, George Mkuchika alisema nchi ambayo Bunge linasumbuliwa na tatizo la rushwa haiwezi kupata maendeleo.

Mkuchika alisema nchi nyingi duniani, taasisi za usalama, mahakama na watu wa manunuzi wamekuwa wakituhumiwa kwa rushwa kutokana na malalamiko ya mara kwa mara, hivyo lazima tatizo hilo lipigwe vita.

Awali akifungua semina hiyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema atahakikisha ofisi yake inawahimiza wabunge katika majimbo yao, kushirikiana na asasi zinazopambana na rushwa ili kupiga vita tatizo hilo.

Ndugai alisema lazima wabunge washirikiane na wale ambao si wanachama wa APNAC na wengine wa mabunge ya Afrika Mashariki kuhakikisha wanapambana na rushwa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment