Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 8, 2017

DR. SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA JANA


A
 Ni  Rais Mstaafu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na viongozi mbali mbali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kisiwandui katika kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa.
A 1
Ni msafara Maalum wa Vijana wa CCM waliokuwa na Picha ya Maehemu Mzee Abeid Aman Karume na mabango yaliyoandikwa maneno mbali mbali aliyowahi kutoa kama nasaha enzi za uhai wake, wakipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Abdallah (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mahgarib Mh. Ayuob Mohamed.
A 2
 Ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita Aman Abeid Karume akisalimiana na viongozi pamoja na Maafisa wa vikosi na majeshi ya Ulinzi ya Tazania na Zanzibar mara baada ya kuwasili kisiwandui.
A 3
Ni Vijana wa CCM wakiwa katika hali ya ukakamavu na wakitembea kwa Mwendo wa haraka huku wakiwa Picha ya Maehemu Mzee Abeid Aman Karume pamoja na  mabango yenye ujumbe unaohusu siku ya mashujaa.
A 4
 Ni Mke wa Aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Kiongozi Mkuu wa ASP Marehemu Mzee Karume, Mama Fatma Karume.
A 5
 Ni Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt. Abdallah Juma Abdallah alipowasili Kisiwandui.
A 6
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)) Generali Venance Mabeyo akisalimiana na viongozi mbali mbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdallah Juma Abdallah alipowasili Kisiwandui.
A 7
Baadhi ya Wazee wa CCM pamoja na viongozi wa Chama na serikali wakisoma hitima katika dua ya kuwaombea Mashujaa.
A 8
 Makamo wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Mh. Samia suluhu Hassan akiwasili katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa.
A 9
 Baadhi ya Mawaziri wa SMZ wakisikiliza mawaidha yaliyokuwa yakitolewa katika hitima hiyo.
A 10
 Ni Makamo wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiweka mashada ya maua ya heshima katika kaburi la Marehemu Mzee Karume, kwa niaba ya Rais wa Jamguri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
A 11
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiweka mashada ya maua ya heshima katika kaburi la Marehemu Mzee Karume. PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
BAADHI ya  Waasisi wa ASP, Wasomi na Viongozi wa serikali na kidini walioudhuria maadhimisho ya kumbumbuku ya Mashujaa Zanzibar, wamesema fursa na mikakati iliyoachwa na Mzee Karume inatakiwa kuwekwa Kisheria ndani ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, ili serikali yoyote itakayoongoza nchi itekeleze kwa vitendo.
Walieleza kwamba miongozo na fursa za kiuchumi, kijamii na kimaendeleo ilichoachwa na Marehemu Mzee Karume inayotekelezwa kwa sasa  haitoshi kubakia katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 bali inatakiwa iwekwe rasmi katika Katiba ya nchi ambayo ni sheria mama ya serikali yoyote inayoingia madarani.
Wito huo ulitolewa na wananchi hao mara baada ya Dua ya hitima ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa ambao ni waasisi wa ASP waliokomboa Zanzibar toka katika Utawala wa Kisultani, iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein huko Katika Makao Makuu ya ASP ambayo kwa sasa ni Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar eneo alilozikwa Mzee Karume.
 Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa amesema kiongozi Mkuu wa harakati za Ukombozi wa Zanzibar Mzee Karume, ameacha urithi wa Hazina ya fikra na mawazo ya maendeleo yanayotakiwa kuendelezwa na vizazi vya sasa na vijavyo.
Waziri Mkuu huyo amekiri kwamba miaka nane ya utawala wa Kiongozi huyo uliwatoa Wananchi kwenye giza la uonevu na mateso na kuwaweka kwenye mwanga wa mafanikio ya kimaendeleo yanayoendelezwa kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Saba Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa nasaha zake kwa wananchi amewasihi kuendelea kuunga mkono serikali iliyopo madarakani kwani ndiyo inayosimamia na kutekeleza, fursa zilizoachwa na Waasisi wa ASP waliowekewa siku maalum ya kitaifa kukumbukwa kwa kusomewa dua kutokana na juhudi zao za kukomboa nchi.
Alisema kuwa Zanzibar itaendelea kuimarika kiuchumi endapo kila mwananchi bila ya kujali itikadi za kisiasa na kidini ataweza kulinda amani, utulivu na kuchukia kwa vitendo tabia ubaguzi, kama ilivyokuwa kwa mashujaa wa ASP walivyoondosha utawala wa mabavu.
“ Leo tumeadhimisha kumbukumbu ya mashujaa wetu lakini bado tuna kazi kubwa ya kulinda na kuendeleza urithi wa Wazee wetu kwani bado, zipo choko choko za baadhi ya watu wenye nia ya kuchafua amani ya nchi yetu lakini na sisi wajue tupo imara kama wazee wetu walivyokuwa mashujaa na kutetea maslahi ya wanyonge”, alielea Waziri Aboud.
Pia Mwenyekiti wa Chama Cha Wakulima (AFP) Zanzibar, Said Soud  Said amesema kazi aliyofanya Mzee Karume ndio iliyozaa matunda ya wazanzibar kuishi kwa utulivu na kujiamulia mambo yao wenyewe.
Amesema ukombozi wa Zanzibar wa mwaka 1964 aliousimamia yeye ndio hasa kioo cha Wazanzibar Duania nzima kujiona kuwa wapo huru na wenye uwezo wa kujenga taifa lao kiuchumi bila vikwazo vyovyote.
Soud ambaye pia ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum  wa  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, alisema baada ya mapinduzi hayo Mzee Karume aliweka misingi iliyofuatwa na viongozi waliotawala baada yake ambayo kwa sasa wananchi wote wa Zanzibar wananufaika nayo.
Aidha kwa upande wake Bi. Asha Simba Makwega aliyelelewa na Mzee Karume na baadae akawa kada wa Afro Shiraz Party(ASP), alisema kwamba kiongozi huyo alitumia muda wake kushughulikia kero na matatizo ya wananchi kuliko muda alioutumia kwa familia yake, hali inayothibitisha uzalendo na utaifa wa kweli wa shujaa huyo.
Sambamba na hayo Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha ADA TADEA, Juma Ali Khatib, alithibitisha utekelezwaji wa falsafa ya Mzee Karume ya Wazanzibar kujitawala kwa Nyanja zote zikiwemo kielimu, kiafya, kimiundombinu, kiutendani na kiutawala na kueleza kuwa dhana hizo zinatekelezwa kwa vitendo na serikali ya Awamu ya saba inayoongozwa na Dkt. Shein.
“ Sote ni mashahidi kuwa serikali zilizopita zimefanya kadri zilivyojaaliwa hata katika Mfumo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa, tulishuhudia baadhi ya viongozi wa upinzani ndani ya mfumo huo walikuwa wakishutumu na kulaumu serikali ambayo na wao walikuwa ni washirika wa kufanya maamuzi jambo ambao katika siasa za kimaendeleo halina mashiko.”, alisema Waziri Ali ambaye pia ni Waziri asiyekuwa na wizara maalum wa SMZ na kumsifu Rais wa Zanzibar Dkt. Shein kwa kufananisha utendaji na busara zake kuwa ni sawa na za Mzee Karume kwani bila ya kujali Dkt. Shein aliteuwa vyama vitano vya upinzani kuingia katika serikali yake kwa lengo la kutengeneza umoja na utaifa wa kwa kweli na kuondosha ubaguzi wa itikadi za kisiasa.
Naye Dkt. Moses John amesema kazi iliyobaki baada ya Mzee Karume kuacha misingi imara ya kuleta uhuru wa nchi, vijana wanatakiwa kusoma kwa bidii ili wapate ujuzi na utaalamu wa kuendesha nchi kisomi kulingana na wakati uliopo sasa ili kuenzi fikra za mashujaa hao kwa vitendo.
Viongozi mbali mbali wa kitaifa wameudhuria maadhimisho hayo wakiwemo Makamo wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samia Suluhu Hassan aliyemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu  Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd,  waziri waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki, Balozi dkt. augustine mahiga, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Said Hassan Said na viongozi wengine  mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na wakurugenzi. 
Pia Viongozi wengine ni Mke wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ya jamhuri Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya sita wa SMZ Aman Abeid Karumr, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwena Mwema Shein, Makamo wa Rais mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed  Gharib bilal, Spika wa Baraza la wawakilishi  Zanzibar  Zubeir Ali Maulid, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Abdallah, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara  ya Itikadi na Uenezi  Bi. Waride Bakari Jabu.
Kwa upande wa viongozi wa dini na mabalozi kutoka nchi mbali mbali walioudhuria ni pamoja na Mufti Mkuu wa Zanzibar Shein Saleh Omar Kaabi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Hassan Ngwali, Askofu wa Kanisa Katoliki Zanzibar Augostino Shao, Balozi mdogo wa msumbiji Jorge augusto, mwakilishi wa balozi mdogo wa China Cheng Kun, Balozi mdogo wa Oman na Mwakilishi wa shirika la kimaifa la UNICEF Tanzania.
Hitima hiyo ilikamilishwa na dua  za Viongozi wa madhehebu mbali mbali ya dini yaliyopo  nchini baada ya kuzuru kaburi la Mzee Karume ambapo kwa upande wa dini ya kiislamu aliyesoma dua  ni Mufti  Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi ambapo madhehebu ya Kikiristo aliyesoma ni Askofu wa Kanisa katoliki Augostino Shao sambamba pia dhehebu la kihindi nao walisoma dua hiyo ya kuwaombea mashujaa hao.
Maadhimisho hayo ya siku ya mashujaa uadhimishwa kila ifikapo  April 7 ya Kila mwaka,  ambayo ndio siku aliyouliwa Mzee Karume na wapinga maendeleo,  Mungu azilazu roho za mashujaa wote walioipigania Zanzibar mahala pema peponi Amin.
Na Mjengwa Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment