UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Thursday, March 30, 2017

Tanzania yawa ya nne kati ya Nchi 44 kwenye hili...


Tanzania imeshika nafasi ya pili  kati ya nchi arobaini na nne zinazopiga hatua kwenye matumizi ya teknolojia katika shughuli za maendeleo barani Afrika hali iliyotokana na watanzania  kupata mwamko mkubwa wa kutumia teknolojia katika shughuli za maendeleo ya kila siku.

Kauli hiyo imesemwa na watalaam wa masuala ya sayansi na teknolojia katika uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya teknoljia katika shughuli za maendeleo  iliyofanyika kwenye taasisi ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela ambapo katika ripoti iliyo zinduliwa nchini Senegal inaonesha Tanzania imeshika nafasi ya pili ikitanguliwa na nchi ya Moroco.

Mwenyekiti wa Chama cha Hisabati Tanzania Emmanuel Kisongo,amesema tafiti pia zinaonyesha kuwa bara la Afrika bado liko nyuma katika matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu  katika kukuza uchumi  wa nchi pamoja na watu wake ukilinganisha na nchi zilizoendelea. 

Mratibu wa Mradi unaosimamia tafiti hizo kutoka shirika la African Capasity Building Foundation (ACBF) la nchini Zimbabwe,Dkt.Michael Haule amesema  Tanzania kupitia  taasisi ya Nelson Mandela imeweza kunufaika na mradi huo muhimu kwa maendeleo ya binadamu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment