Writen by
sadataley
1:25 PM
-
0
Comments
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa
usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Shirika la Umeme
nchini (Tanesco).Mradi huo umezinduliwa rasmi kitaifa katika kijiji cha
Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga.
.Wakazi wa kijiji cha Zingibari
Wilayani Mkinga mkoani Tanga wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ( hayupo pichani) wakati wa
uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na
Tanesco.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Dkt. Medard Kalemani,(katikati), Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela(
kushoto) na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, Mhaga Mpina(kulia) wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga,
Mawaziri hao walikuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Dkt. Medard Kalemani, akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Zingibari
wilayani Mkinga mkoani Tanga alipofika kijijini hapo kuzindua rasmi
mradi wa usambazaji wa umeme vijijini kitaifa unaotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Tanesco.
Na Zuena Msuya, Tanga
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme
vijijiji ,unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya
Tatu kitaifa kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco,utakao
sambaza umeme kwa vijiji vyote ambavyo havikupata huduma hiyo wakati wa
REA Awamu ya Kwanza na ya Pili.
Akizungumza katika uzinduzi huo
uliofanyika katika kijiji cha Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga,
Dkt . Kalemani alisema kuwa, REA Awamu ya Tatu itatekelzwa kwa miaka
mitano kuanzia sasa hadi kufikia 2021.
Dkt. Kalemani alifafanua kuwa,mara
baada ya uzinduzi rasmi wa kitaifa wa mradi huo mkoani Tanga,Mikoa
mingine itaendelea kuzindua mradi huo katika mikoa yao kulingana na
makubaliano ya mikataba ya wakandarasi husika katika Mikoa hiyo.
“REA awamu ya Tatu imezinduliwa
rasmi hapa mkoani Tanga, mradi huu sasa utamaliza kazi ya kuunganisha
huduma ya umeme katika vijijini vyote 7867 nchini vilivyoachwa katika
Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi huo, ili kifikia idadi ya vijiji
vyote 12,262,Tanzania bara ifikapo mwaka 2021”, alisema Kalemani.
Akizungumzia mradi huo kwa Mkoa wa
Tanga, Dkt. Kalemani alisema kuwa REA Awamu ya Tatu itasambaza huduma
ya umeme katika vijiji 166, ambapo vijiji 20 kati ya hivyo ni vile
ambavyo vilipitiwa na Mradi wa REA Awamu ya Kwanza na ya Pili lakini
havikuunganishwa na huduma ya umeme , na vijiji 146 ambavyo havikupitiwa
kabisa wala kuunganishwa na Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini
iliyopita.
Aidha , Dkt. Kalemani alitoa wito
kwa wakandarasi watakaotekeleza Mradi wa REA Awamu ya Tatu, kutekeleza
majukumu yao kwa wakati kwa kuzingatia uhitaji wa huduma ya umeme nchini
ili kutimiza azma ya Serikali ya kuwa nchi ya viwanda.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Martin Shigela aliwataka wakazi wa Mkoa huo waliokosa huduma hiyo
katika miradi iliyotangulia, kutandaza nyaya za umeme katika nyumba zao
ili kuweza kuunganishwa na huduma ya umeme ambayo hupatikana kwa bei
nafuu ya shilingi elfu 27 .
Aidha aliwataka wananchi hao
kulinda na kuitunza miundombinu ya mradi huo kwa maslahi ya taifa na
wananchi kwa ujumla kwa kuwa miundombinu hiyo ni ya gharama kubwa.
No comments
Post a Comment