Writen by
sadataley
12:52 PM
-
0
Comments
Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya makombora manne
China imependekeza kwamba Korea
Kaskazini ipige marufuku majaribio yake ya makombora pamoja na
teknolojia yake ya nyuklia ili kuzima wasiwasi unaoendelea.
Waziri wa maswala ya kigeni Wang Yi
alisema kuwa kwa makubaliano hayo Marekani na Korea Kusini zitasitisha
mazoezi ya kijeshi ya pamoja ambayo yanakasirisha Korea Kaskazini.
Ombi hilo linajiri baada Korea Kaskazini
kufanyia majaribio makombora yake manne siku ya Jumatatu na kukiuka
vikwazo vya kimataifa.
Ili kujibu hatua hiyo, Marekani imeanza kuweka mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Thaad.
Akizungumza kando kando ya mkutano wa
kila mwaka wa bunge, bwana Wang alisema kuwa mgogoro huo wa Korea ni
kama treni mbili zinazokwenda katika barabara moja huku zote zikikataa
kutoa nafasi kwa mwengine kupita.
"je pande hizi mbili ziko tayari kugongana?,aliuliza.
''Usitishaji wa operesheni za kijeshi
baina ya mataifa haya utakuwa hatua ya kwanza katika kumaliza wasiwasi
na kuanzisha majadiliano'',alisema.BBC
No comments
Post a Comment