Writen by
sadataley
1:12 PM
-
0
Comments
Wanahabari mkoa wa Iringa
walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa katika picha
ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tatu
kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha
iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari
kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa.
Wanahabari mkoa wa Ruvuma
walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa katika picha
ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tatu
kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha
iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari
kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa
Meneja mahusiano wa Shirika la Maendeleo
ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu (TPDC) akitoa neno wakati
wa utangulizi wa warsha hiyo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya
Iringa,Njombe na Ruvuma.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard
Kasesela amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha,
Iringa,Ruvuma na Njombe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo
ya siku moja ambayo yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja
mwaka huu(21 / 02 /2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.
“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda
kulipongeza Shirika letu la Mafuta la Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo
vya habari katika kupata uelewa mpana wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi
ili waweze kuhabarisha na kuelimisha watanzania kwa ujumla ili watambue
shughuli za shirika na faida zake haswa katika uchumi wa nchi”, alieleza
Mkuu wa Wilaya.
Aidha Mh Kasesela amewaomba Waandishi wa
Habari kuwa wazelendo katika kuisaidia Serikali kutekeleza miradi
mbalimbali yenye maslahi mapana katika maendeleo ya nchi yetu.
‘’Waandishi Wahabari mnapaswa kuisaidia
Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija kwa uchumi
wa Taifa, mfano katika vita ya kiuchumi ya kugombania mradi wa bomba la
mafuta ghafi kutoka Uganda kati ya Tanzania na Kenya, wenzetu Kenya
walijitahidi kuandika habari zenye kutoa wasifu wa nchi yao ili
kuisaidia kupata mradi huo, hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya kazi
kiuzalendo.”
Aliongeza kuwa leo hii mmeweza kuifahamu TPDC sasa mnapaswa kuwaeleza wananchi miradi inayofanywa na Shirirka hili na manufaa yake katika uchumi wa Taifa, mwende mkatafiti namna mradi wa bomba la mafuta utakavyonufaisha wananchi wanaoishi kando ya njia ya bomba hilo, vilevile namna bomba hilo litakavyosaidia kukuza uchumi wa nchi, hivi ndivyo tunavyoweza kujenga nchi yetu kupitia taaluma ya uandishi wa habari.
Kasesela alisisitiza kuwa ili tujenge Taifa imara ni vyema tuandike habari kwa weledi, uzalendo huku tukiondoa tofauti zetu za kiitikadi ziwe za kikabila, kisiasa au kidini kwa namna hii tutaweza kuandika habari zenye kujenga nchi yetu na si vinginevyo.

Alisisitiza vile vile juu ya utoaji
taarifa mapema pale mtu anapoona kuna hujuma au uharibifu wa aina yoyote
katika miundombinu hii, akiongea katika warsha hiyo alisema
“miundombinu hii ya gesi na mafuta ni mali ya watanzania hivyo kuilinda
ni jukumu letu sote kama wazalendo wa nchii hii”.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha
hiyo, Afisa mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi
Tanzania Maria Mselemu alisema warsha hii inalenga kuendelea kuwajengea
uwezo zaidi waandishi wetu wa habari kuweza kuripoti kwa umahiri na
ustadi habari za mafuta na gesi.
Mselemu aliwashukuru waandishi wa habari
kwa juhudi zao za kuupasha habari umma na kuwaasa kwamba kalamu yao ina
nguvu hivyo ni vyema ikaendelea kutumika kujenga uchumi wa Taifa kwa
kutoa taarifa sahihi kila wakati.
Katika taarifa yake Faustin Kayombo kutoka mkondo wa juu (TPDC) alisisitiza juu ya matarajio yasiyo halisia yaliyopo miongoni mwa wanajamii na kuwaomba waandishi wa habari kusaidia kuwaeleza wananchi juu ya uhalisia wa sekta.

Kayombo alisema kwamba uwekezaji katika
sekta ya mafuta na gesi ni wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana
ya mapato makubwa kwa Serikali huchukua muda mrefu kuonekana.
Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Kayombo alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.

Hata hivyo Kayombo alisisitiza juu ya ushiriki wa wazawa katika sekta hii hususan katika kutoa huduma na kuuza bidhaa.
Naye mwanasheria wa TPDC Barnabas
Mwashambwa alisema sheria mpya ya petroli ya mwaka 2015 inawataka
wawekezaji wote kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kama
ikitokea bidhaa hizo hazipo nchini basi kampuni iingie ubia na kampuni
ya kizawa ili kuweza kutoa huduma inayohitajika.
Sheria imeeleza kwamba ubia huo lazima
umpe mzawa ushiriki usiopunguza asilimia 25%, hii ni fursa kwa wazawa na
ni vyema ikachangamkiwa.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa frank leornad ameliomba Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutenga muda wa kutosha zaidi katika uelimishaji ili walengwa waweze kuelewa vyema sekta, ombi ambalo liliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya.
Katika mafunzo hayo waandishi wa habari walipata fursa ya kujifunza kuhusu maendeleo ya Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Gesi Asilia na Faida Zake, Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanga na Usambazaji wa Gesi Asilia Majumbani, Viwandani na kwenye Vituo vya Kujaza Magari.

TPDC imeendelea kutoa elimu kwa wadau
mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa zaidi katika sekta hii mpya
na changa ya mafuta na gesi hapa nchini.
Chanzo: Mjengwa Blog
No comments
Post a Comment