Writen by
sadataley
10:45 AM
-
0
Comments
Bw Nahimana (kushoto) akiwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mwaka jana ambapo alizuiwa kwenda Rwanda
Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.
Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.
Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
wenyewe
Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri ni wafungwa wanaotumukia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama vile kukanusha kuwa mauwaji ya kimbari hayakufanyika nchini Rwanda mwaka 1994.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda
No comments
Post a Comment