Writen by
sadataley
10:58 AM
-
0
Comments
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema anakubaliana na sera ya Rais wa
Marekani Donald Trump kwamba "Marekani iwe ya Wamarekani".
Hata hivyo, amesema hakutaka pia "Madam Clinton ashinde", akirejelea mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton.
Ameongeza kwamba Bw Trump anafaa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake.
"Sijui. Mpeni muda. Bw Trump huenda hata labda ataangalia upya vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe," Bw Mugabe amesema.
Mahojiano kamili ya Bw Mugabe yanatarajiwa kupeperushwa rasmi kesho jioni kwenda sambamba na maadhimisho ya kusherehekea kiongozi huyo kutimiza miaka 93 tangu kuzaliwa kwake
Bw Mugabe ameongoza Zimbabwe nchi hiyo tangu uhuru mwaka 1980.
(chanzo BBC)
No comments
Post a Comment