Writen by
sadataley
1:34 PM
-
0
Comments
Mvua zilizoanza kunyesha wilayani Monduli mkoani Arusha zimesababisha mawasiliano ya barabara katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo kukatika, baadhi ya wananchi kukosa huduma na pia wanafunzi kushindwa kwenda shule kutokana na baadhi ya mito kufurika.
Wananchi na viongozi wa maeneo yaliyoathiriwa na hali hiyo wamesema tatizo hilo ni la muda mrefu na ni jambo la kawaida wakati wa msimu wa mvua unapoanza na ni kubwa zaidi katika tarafa ya Makuyuni.
Hali hiyo pia imeshudiwa na viongozi watendaji na wataalam wa wilaya na mkoa ambao walilazimika kukatisha safari ya kwenda kusikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Oltukai wanaokabiliwa na matatizo mbali mbali likiwemo tatizo la maji.
Wakizungumzia hali hiyo viongozi hao akiwemo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Monduli Bw. Steven Ulaya na mwenyekiti wake Bw. Issack Joseph wamesema tatizo hilo ni kubwa katika wilaya hiyo na kwamba wanafunzi wote wanalazimika kulala shuleni.
Baada ya msafara wake kukwamishwa na mafuriko hayo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka watendaji wa halmashauri hiyo wakiwemo watalaam kuanda mpango wa muda mrefu wa kukabiliana na hali hiyo ili kuepuka madhara yasiyo ya lazima.

No comments
Post a Comment