Writen by
sadataley
1:29 PM
-
0
Comments
Mechi hiyo itakayofanyika kesho kutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.
Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyofanyika Oktoba Mosi mwaka jana,
timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, Shiza Kichuya akiisawazishia Simba
katika dakika ya 87.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina,
alisema kuwa kikosi chake kimeiva na wanachosubiri ni kutekeleza
maelekezo waliyowapa ya kusaka pointi tatu muhimu.
Lwandamina ambaye mechi yake dhidi ya Simba kwenye mashindano ya Kombe
la Mapinduzi alikubali kichapo, alisema kuwa anataka kuona wanaibuka na
ushindi ili safari yake ya kutwaa ubingwa na Yanga kuweka rekodi ya
kushinda taji la Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo wanalitimiza.
"Ni mechi kubwa na muhimu kwa kila upande, ila Yanga tutaingia uwanjani
tukifahamu tunachokwenda kukifanya, ushindi ndiyo jambo tunalolitarajia,
tunataka pointi tatu muhimu," nahodha msaidizi wa Yanga na kiungo wa
kimataifa kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima alisema jana.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Salum Mkemi, alisema
kila mchezaji amejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo huo na kuhakikisha
timu yake inaondoka na ushindi mnono ili kulinda heshima yao, viongozi,
wanachama pamoja na timu yao.
“Tutaifunga Simba magoli mengi sana, na mwaka huu ni lazima ishuke
daraja kwa sababu tutawafunga magoli mengi kipindi cha kwanza, hivyo
hawatarudi kipindi cha pili na kwa sheria za TFF ( Shirikisho la Soka
Tanzania), timu isiporudi uwanjani inashushwa daraja,” alisema.
Kuhusu hali ya straika, Donald Ngoma, kuwa katika hatihati ya kutocheza
mechi hiyo, kiongozi huyo alisema hawana wasiwasi wowote kwa sababu
kikosi chao kina washambuliaji wengi wenye uwezo wa kuifunga Simba.
Aliongeza kuwa benchi la ufundi la Yanga linamuandaa mshambuliaji huyo
kutoka Zimbabwe kwa ajili ya kuwavaa Zanaco katika mechi ya mashindano
ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika Machi 11 hapa jijini na
marudiano wiki moja baadaye huko Lusaka, Zambia.

No comments
Post a Comment