Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, February 22, 2017

AMNESTY WAMSHUKIA RAIS TRUMP NA VIONGOZI WAKE

Amnesty inataja matamshi ya Bw Trump kama "Kampeini yenye sumu"  Amnesty inataja matamshi ya Bw Trump kama "Kampeini yenye sumu"                
Shirika la Amnesty International limemshutumu Rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wengine nchini Uturuki, Hungary na Ufilipino.
Shirika hilo limesema viongozi hao wanaendeleza kile inachokitaja kuwa kuwatumia vibaya wakimbizi, kwa manufaa yao ya kisiasa, badala ya kutanzua kiini hasa kilichowafanya wakimbizi hao kuyakimbia mataifa yao.

Katika ripoti yake ya kila mwaka, Amnesty inaelezea mwaka 2016, kama mwaka wa matamshi yaliyojaa chuki huku hofu ikapanda zaidi na kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikia tangu miaka ya 1930, wakati Adolf Hitler, alipoingia uongozini nchini Ujerumani.

Amnesty inaikosoa pakubwa jamii ya kimataifa kuhusiana na namna inavyoshughulikia mzozo wa wakimbizi nchini SyriaHaki miliki ya picha AFP
  Amnesty inaikosoa pakubwa jamii ya kimataifa kuhusiana na namna inavyoshughulikia mzozo wa wakimbizi nchini Syria
Ripoti hiyo inapinga sera ambazo zinakubalia ubaguzi wa rangi na chuki.
Inasema mataifa mbalimbali duniani yanaendesha ajenda potovu ambayo inawahujumu wakimbizi ambao wanashutumiwa kwa makosa ambayo hawakutenda huku pia wakidhulumiwa kijumla.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment