Writen by
sadataley
2:23 PM
-
0
Comments
Makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Jumatatu mjini Addis Ababa Ethiopia kwa msaada wa wapatanishi kutoka Jumuiya ya maendeleo ya serikali za kanda ya Afrika Mashariki IGAD.
Hakuna upande uliotoa maelezo ya kina kuhusu makubaliano hayo lakini wamesema watakutana tena Februari 20 kukamilisha maswala yote kwenye mkataba huo.
Wote, Kiir na Machar wametia saini mikataba mingine hapo awali lakini ikavunjika. Mpatanishi wa IGAD Seyoum Mesfin alionya kuwa yeyote atakayevunja makubaliano yaliyotiwa saini hivi karibuni, ataripotiwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
No comments
Post a Comment