Writen by
sadataley
8:07 AM
-
0
Comments
Michuano ya Vilabu Afrika yapamba moto
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho, timu za Azam na Yanga zimeanza vema safari yao ya kuwania makombe hayo baada ya kila timu kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao.
Timu ya Yanga wawakilishi katika Kombe la Shirikisho, Jumamosi waliwacharaza wawakilishi wa Botswana, BDF kwa kuwachapa magoli 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Magoli ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji wake Amis Tambwe katika kila kipindi cha mchezo, ambapo bao la kwanza lilifungwa mapema mno katika sekunde ya 57 ya mchezo.Ushindi huo unairahisishia Yanga kusonga mbele katika mchezo wa marudiano utakaofanyika mjini Gaborone wiki mbili zijazo.
Mabao ya Azam yalifungwa na Didier Kavumbagu na John Bocco.
Azam wanatarajiwa kurudiana na El-Merreikh mjini Khartoum, wiki mbili zijazo.
Sofapaka ya Kenya nayo imepoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Platinum ya Zimbabwe kwa kuchapwa magoli 2-1. Rayon Sport ya Rwanda imepata ushindi ugenini kwa kuifunga Panthere ya Cameroon goli 1-0. Nayo URA ya Uganda imepata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Elgeco Plus ya Madagascar.
Mbali na Azam ya Tanzania kupata ushindi katika mchezo wake wa awali dhidi ya Al-Marreikh, katika michezo ya Klabu bingwa Afrika, Kampala City Council ya Uganda imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cosmos de Bafia ya Cameroon, wakati Gor Mahia ya Kenya ikicharaza CNaps Sport ya Madagascar goli 1-0.
No comments
Post a Comment