Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, January 28, 2015

Profesa Lipumba awekwa kizuizini

   
Profesa Ibrahimu Lipumba,Mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF Tanzania
Polisi Tanzania linamshikilia mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba na wakiwemo wafuasi wake 32 pia kwa tuhuma za kufanya maandamano yanayodaiwa kuwa si halali.
Inadaiwa kuwa polisi hao awali walizuia maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika kama sehemu ya maadhimisho ya kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso kwa baadhi ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro ameiambia BBC kuwa wanamshikilia mwenyekiti huyo wa Chama cha siasa cha CUF na kwamba kati ya hao 32 wanaoshikiliwa wawili ni wanawake.
Polisi kwa mjibu wa Siro wanasema walikwisha waandikia barua barua viongozi wa chama hicho cha CUF kupinga kufanyika kwa maandamano hayo kwa sababu za kiusalama
Mwak 2001 chama cha CUF visiwani Zanzibar waliendesha maandamano yaliyosababisha baadhi ya Polisi na raia kadhaa kufa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment