Writen by
sadataley
3:11 PM
-
0
Comments
Yaya apatikana na hatia Uganda
Yaya wa Uganda ambaye alinaswa kwa kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto mdogo amepatikana na hatia ya ukatili.
Atafikishwa mahakamani tarehe 15 Jumatatu Disemba kupokea hukumu .Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa alilazimika kufanya kitendo chake kwa sababu mamake mtoto huyo aliwahi kumchapa mara kadhaa.
Alipokuwa anaondoka kortini mamake mtoto Angella Mbabazi, alikanausha madai ya Jolly akisema hajawahi kumgusa Jolly hata wakati mmoja.
Alihoji madai ya Jolly akisema angewezaje kumchapa msichana huyo wa kazi na kisha amuache na mtoto wake?
Awali tuhuma dhidi ya Jolly kuwa alimtesa mtoto huyo, yalitupiliwa mbali na mwendesha wa mashitaka wakisema ingekuwa vigumu ,kuweza kuyathibitisha
Huenda akafungwa jela miaka 5 jela kwa kumchapa na kumjeruhi mtoto.
No comments
Post a Comment