Writen by
sadataley
2:34 PM
-
0
Comments
Wakaazi wanaolala bila kujua Kazakhstan
Ugonjwa wa ajabu unaowafanya raia wa kijiji kimoja kulala kwa siku kadhaa unasababishwa na kuwepo kwa maji mengi katika ubongo kulingana na madaktari.
Madaktari hatahivyo wameshindwa kubaini chanzo cha ugonjwa huo ambao umeawaathiri wanakijiji cha Kalachi kazkazini mwa Kazakhstan kwa zaidi ya miaka minne.Wakaazi wanasema kwamba ugonjwa huo wa kushangaza unaendelea kuwaathiri huku ikiwa asilimia 14 ya wakaazi 600 wa mji huo wameathiriwa.
Katika msimu wa joto,takriban watu 60 walipelekwa hospitali wakiugua ugonjwa huo ambao huwaacha waathiriwa wakisikia kisunzi,kushindwa kusimama,uchovu pamoja na tatizo la kukumbuka.
Wengine wameripoti kukumbwa na ndoto za maajabu.
Tayari madaktari wamepinga kuwepo kwa virusi ama bakteria kama sababu ya ugonjwa huo.
Wanasayansi pia wameshindwa kupata kemikali zozote katika mchanga ama hata maji ambazo pengine huenda ndizo zinazosababisha ugonjwa huo wa kulala.
Baadhi ya wakaazi katika kijiji hicho ambacho kiko maili 276 kutoka mji mkuu wa Kazakh, Astana sasa wanaishi kwa hofu kwamba huenda wasiamke tena kutokana na ugonjwa huo.
No comments
Post a Comment