Writen by
sadataley
5:42 PM
-
0
Comments
Uchaguzi wa masineta wafanyika Liberia
Shughuli za upigaji kura zinaendelea nchini Liberia kuwachagua maseneta wapya licha ya kuwepo kwa hofu kwamba kura hiyo huenda ikachangia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.
Uchaguzi huo umehairishwa mara kadha lakini rais Ellen Johnson - Sirleaf anasema kuwa kura hiyo ni lazima ifanyike wakati huu ili kuzuia msukosuko .Mikutano ya kisiasa ilipigwa marufuku kufuatia hatari iliyotokana na ugonjwa wa ebola ambao umewaua maelfu ya watu magharibi mwa afrika.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi nchini Liberia wanaamini kuwa kura hiyo ni hatari sana na kesi ya kuizuia isifanyike imepelekwa kwenye mahakama ya juu.
No comments
Post a Comment