Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Friday, November 7, 2014

Waandamana kupinga sera,Ubelgiji

   
Waandamanaji Belgium
Polisi nchini Ubelgiji katika mji mkuu BrusselsUbelgiji wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na maji ili kuwatawanya waandamanaji wanaopinga sera ya kutaka kuongeza muda kustaafu kwa watumishi wa umma pamoja na kupunguza bajeti ya huduma za jamii
Waandamaji hao ambao pia walikuwa wakiwasha moto, wameunguza magari,wamerusha mawe na uharibifu mwingine.
Serikali ya umoja wa kitaifa ya Ubelgiji inasisitiza kuwa mabadiliko yanahitajika na kwamba mabadiliko hayo yanapaswa kupunguza tofauti ya mahitaji ya bajeti ili kuendana na miongozo ya jumuiya ya Ulaya.
Machafuko nchini humo yalianza mwezi marchi mwaka huu pale waandamanaji kwa mara ya kwanza walioingia mitaani wakiwa na mabango yanayopinga baadhi ya sera nchini humo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment