Writen by
sadataley
7:59 AM
-
0
Comments
RC IRINGA AKABIDHI MIFUKO YA SARAJI 115 KWA MANISPAA YA IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma (wa pili kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Leticia Warioba jana kabla ya kukabidhi msaada wa mifuko 115 ya sementi yenye thamani 1,725,000/- kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari. Wanaoshuhidia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Ayub Wamoja (kulia) na mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
Na FRIDAY SIMBAYA, IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma jana amekabidhi msaada wa mifuko 115 ya sementi yenye thamani 1,725,000/-kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.
Dkt. Ishengoma kwa kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa ametoa mifuko ya sementi hiyo ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara na kuwataka wananchi na taasisi mbalimbali kujitolea kuchangia ujenzi huo ili kuongeza kasi ya kuzalisha walimu wa masomo ya sayansi.
Alisema kuwa ujenzi wa maabara katika shule za sekondari ni utekelezaji wa agizo la rais aliyezitaka shule zote za sekondari nchini kuwa na maabara tatu kwa kila shule.
Akipokea msaada huo wa vifaa vya ujenzi mkuu wa wilaya iringa, Leticia Warioba kwa niaba Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo aliwaomba wadau mbalimbali yakiwemo mashirika, taasisi, watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kujitokeza kuchangia ujenzi wa maabara.
Warioba alisema kuwa ili kufanikisha malengo ya wilaya ya iringa inahitaji michango ya wadau mbalimbali ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyezitaka halmashauri zote kuhakikisha zinajenga maabara katika shule za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo alisema manispaa hiyo inahitaji maabara za kudumu 28 na hadi sasa kuna jumla ya maabara 22 zinaendelea kujengwa na maabara sita ziko katika hatua ya mwisho kukamilika.
Hata hivyo, maabara zinazoendelea kujengwa katika manispaa hiyo ni pamoja na vyumba vya maabara ya fizikia, kemia na baiolojia ifikapo mwaka 2016.


No comments
Post a Comment