Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, November 8, 2014

PAPA ATEUA ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU KANISA KATOLIKI DODOMA

Na Frederic M. Gabriel
wa Globu ya Jamii  
                         
Askofu Beatus Kinyaiya


Hatimaye Baba Mtakatifu Papa Francisco wa kanisa Katoliki duniani amempandisha kutoka Askofu hadi kuwa Askofu Mkuu Askofu Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap (pichani) wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma.

Baba Askofu Beatus Kinyaiya alizaliwa Mei 9, 1957. Akapata daraja takatifu la Upadre katika shirika la Kimisionari la Wafranciscan Minor tarehe 25 juni, 1989.

Aliteuliwa kuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Mbulu tarehe 22 Aprili, 2006, na kusimikwa/ kuwekwa wakfu rasmi na Kardinali Polycarp Pengo kuwa Askofu wa jimbo la Mbulu Julai 2, 2006.

Na tarehe Novemba 6, 2014 ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dodoma ambalo nalo limepandishwa hadhi na kuwa Jimbo Kuu.

Askofu Beatus Kinyaiya atasimikwa rasmi kuanza utume wake huo mpya katika jimbo hilo mwezi wa Januari, 2015.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment