Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, November 3, 2014

NEEMA CRAFTS WATOA MSAADA WA BASKELI KWA WALEMAVU.

Walemavu Mkoani Iringa wakifurahia baada ya kukabidhiwa baskeli zao ikiwa ni msaada kutoka Neema Crafts. 
Na Simon Victor
Walemavu mbalimbali mkoani Iringa hapo jana walipewa msaada wa baskeli arobaini kutoka Neema Crafts ambao wako chini ya dayosisi ya Ruaha.
Mkurugenzi mtendaji wa Neema Crafts bwana Benjamin Ray akizungumza kwenye makabidhiano hayo alisema kuwa, Neema crafts ilianzishwa mwaka 2003 chini ya dayosisi ya Ruaha.

Kituo kilianza kikiwa na viziwi watatu na walikuwa wakijishungulisha na utengenezaji wa karatasi. Mwaka 2009 walijenga jengo ambalo wanalitumia kwa mgahawa na mwaka 2011 waliongeza jengo jingine ambalo wanitumia kama nyumba ya kulala wageni ambayo inasimamiwa na walemavu na kuwa nyumba ya kwanza ya kulala wageni kusimamiwa na walemavu wa kuongea(Mabubu).
Bwana Ray alisema miradi yao yote inasimamiwa na walemavu wa aina mbali mbali.Pia Ray isema msaada wa baskeli waliotoa kwa walemavu ni zawadi waliyopewa kutoka nchini Marekani katika jimbo la Minnesota.
Nae Mwenyekiti wa Walemavu(CHAWATA) mkoani Iringa Bwana Shaabani Shomari aliwashukuru Neema Crafts kwa msaada waliotoa kwao.Lakini akatatoa angalizo kwa walemavu wote waliopata baskeli hizo wazitumie kwa madhumuni yaliokusudiwa.
Pia Katibu wa CHAWATA Mkoa wa Iringa Ndugu, Haruna Mbata amewapongeza Neema Crafts kwa kuwa bega kwa bega na wao na msaada waliotoa ni chachu kwa maendeleo ya walemavu Mkoani Iringa.
Habari kwa hisani ya Mjengwa blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment