Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, November 6, 2014

Marekani: chama cha Republican chapata wingi wa viti

    
Chama cha Republican kimepata idadi kubwa ya viti katika baraza la Seneti.
Chama cha Republican kimepata idadi kubwa ya viti katika baraza la Seneti.

Na RFI
Nchini Marekani chama cha Republican kinaelekea kupata idadi kubwa ya viti katika bunge la Senate, na sasa wanahitaji viti sita tu ili kudhibiti bunge hilo.

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa chama hicho kimepata ushindi katika majimbo ya Arkansas, Montana, South Dakota na West Virginia.
Kulingana na matokeo ya awali, chama cha Republican kinaongoza kwa viti 51 kwa jumla ya viti 100.
Kiongozi wa chama cha Republican Mitch McConnell, amehifadhi kiti chake katika jimbo la Kentucky na kusema mambo yanavyokwenda inaonesha wazi kuwa raia wa Marekani wana imani na chama cha Republican.
Chama cha Republican pia kimepata ushindi katika majimbo ya Mississippi, Alabama, Maine na South Carolina, huku chama cha rais Barrack Obama Democratic kikiibuka ushindi katika majimbo ya Massachusetts, Rhode Island, Delaware , New Jersey na New Hampshire.
Ikiwa chama cha Republican kitashinda viti vingi, inaaminisha kuwa itakuwa vigumu kwa miswada ya serikali kupitishwa katika baraza hilo la Seneti.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment