Writen by
sadataley
7:15 AM
-
0
Comments
 |
| Msafawa wa jeshi uliobeba mwili wa aliyekuwa rais wa taifa la Zambia, Michael Sata ukitokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth kaunda kuelekea ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mulungushi |
Maelfu ya wananchi wa Zambia wamejitokeaza kwa makundi makundi kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wao, Michael Sata ambaye aliripotiwa kufariki dunia usiku wa tarehe 28 Oktoba jijini London ambalo alienda kwa ajili ya kupatiwa matibabu (
bofya kusoma).
 |
| Rais anayekaimu, Guy Scott akikagua gwaride wakati wakisubiria ndege iliyobeba mwili wa Michael Sata kuwasili |
 |
| Ndege iliyobeba mwili wa Michael Sata ikiwa imesaili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Keneth Kaunda |
 |
| Mjane, Dkt Christine Kaseba akisaidiwa kushika kwenye ndege pamoja na wanafamilia |
 |
| Bi Charlotte Scott, ambaye ni mke wa rais anayekaimu, Guy Scott, akimfariji mjane, Dkt Christine Kaseba |
 |
| Jeneza likiwa tayari kuteremshwa kutoka kwenye ndege |
 |
| Makamanda wa jeshi wakipeleka jeneza sehemu husika kwa ajili ya kusafirisha watu wakatoe heshima zao za mwisho |
 |
| Mizinga 21, heshima kwa aliyekuwa mkuu |
 |
| Jeneza likifungwa vema kwa ajili ya safari |
Mara baada ya mwili wake kuwasili nchini humo na kupokelewa kwa taratibu zote za kijeshi, viongozi wakuu walipata fursa ya kumuaga na kisha kufuatiwa na wananchi, ambapo kwa hivi sasa mwili upo kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mulungushi, wananchi wakiendelea kupewa nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho hadi Jumapili Novemba 9.
Zifuatazo ni picha za matukio kama ambavyo GK imekukusanyia kutoka Lusaka Times...
 |
| Waliowezesha matukio kuwa hewani |
 |
| Gari iliyo na dhamana ya kubeba mwili wa aliyekuwa rais wa Zambia, Michael Sata ikitokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda |
 |
| Waliojitokeza pembezoni mwa barabara ya uwanja wa ndege |
 |
| Jeneza likiwa limewekwa na maafisa wa jeshi kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mulungushi, tayaru kwa wananchi kutoa heshima zao za mwisho, |
Mjane, Dkt Christine Kaseba akatoa heshima zake
 |
| Rais Guy Scott na mkewe wakiaga mwili wa Michael Sata |
 |
| Mjane wa marehemu, Dkt Christine Kaseba (kushoto), Guy Scott na mkewe sanjari na binti wa marehemu (kulia) |
 |
| Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Zambia, Dr Kenneth Kaunda (aliyeinama) pamoja na watoto wa marehemu. |
Nawapeni pole ndugu zetu Wazambia wote na Afrika kwa ujumla kwa kupoteza kiongozi mmojawapo aliyekuwa anategemewa kudumisha amani, umoja na mshikamano kwa taifa hilo ambalo limetamkwa kuwa taifa la Kikristo kwenye katiba yake. Ni muda muafaka kuwaombea ili waepukane na mafarakano.
Habari kwa hisani ya
www.gospelkitaa.co.tz
No comments
Post a Comment