Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Monday, November 10, 2014

JK AENDELEA VYEMA NA MATIBABU ANAYOPATIWA HUKO MAREKANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini Marekani, leo Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume.

Habari kutoka hospitalini hapo zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote ni mswano. Tutaendelea kwuashirikisha taarifa ya maendeleo yake mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani kulijenga Taifa.(PICHA NA IKULU)
Habari kwa hisani ya mtandao wa Godwin Francis
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment