Writen by
sadataley
8:06 AM
-
0
Comments
ukistaajabu ya Musa?
Wakati harakati mbali mbali za kupinga ndoa namimba za utotoni zikiendelea na hasa katika nchi za Africa,baadhi ya nchi barani humo zinakabilia na changamoto hii kupita kiwango.
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni ,Kesi ya kwanza na ya namna yake imeedeshwa na kutolewa hukumu huko nchini I vory Coast baada ya mwanamume mmoja kuamua kumuoa binti yake wa miaka 11.Kutokana na kitendo cha mwanamume huyo kumua binti yake alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na faini ya dola za kimarekani mia saba.
Mwendesha mashtaka Rosine Kone amesema kwamba kesi hiyo ya aina yake itatuma ujumbe mzito kwa raia wa nchi hiyo ili waeme na tamaa zao.
Nao umoja wa mataifa unasema kwamba ndoa za utotoni nchini Ivory Coast si la kushangaza ni kawaida yao,kwani mmoja kati ya mabinti watatu huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka kumi na nane.
No comments
Post a Comment