Writen by
sadataley
9:00 PM
-
0
Comments
Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo.PICHA|MAKTABA
Na Daniel Mjema,Mwananchi
Moshi. Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo ameapa kufanya kampeni angani na ardhini, kuhakikisha kuwa CCM inashindwa vibaya uchaguzi mkuu wa 2015.
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana mjini Moshi, Ndesamburo aliahidi kutoa helikopta yake na kukodi nyingine kutoka nje ya nchi kuendesha kampeni hiyo ya nguvu.
Hata hivyo, Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, alikataa kutaja idadi ya helikopta zitakazokodishwa akisema kufanya hivyo ni kuwapa faida maadui kujipanga kukukabili.
“Nataka niwahakikishie helikopta itaruka katika kila kijiji cha mkoani Kilimanjaro kuhakikisha CCM hakipati jimbo hata moja. Uwezo huo ninao. Sababu ninazo na nia pia ninayo,” alisema na kuongeza:
“2015 Tutawapelekesha mchakamchaka ambao hawajawahi kuuona. Tunaomba wananchi watuunge mkono na tutaanzia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Desemba.”
Kwa mujibu wa Ndesamburo, helikopta hiyo na zingine zitakazokodishwa kama itabidi, zitatumika pia kumnadi mgombea urais atakayepeperusha bendera ya Ukawa katika uchaguzi huo.
Ndesamburo alisema kupitia mwongozo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), watateua wagombea wanaokubalika na wananchi na siyo wanaokubalika na viongozi kama wanavyofanya CCM.
“Safari hii hakuna mgombea kupita bila kupingwa. CCM wajiandae kwa maumivu na wajiandae kwa maumivu makubwa kuliko wanavyofikiri,”alisisitiza Ndesamburo na kuongeza:
“Tumejaribu kutafuta na kujenga uhusiano na vyama vingine vya siasa. Nchi itatikisika kwa matokeo ya uchaguzi huu.”
Alisema CCM walizoea siku zote kuwa harakati za Chadema zinapimwa kwa mikutano ya hadhara na maandamano, lakini Chadema kiliamua kwenda kimya kimya na kujikita kwa wananchi.
“Kitu ambacho hawakukijua ni kwamba tuliacha mikutano ya hadhara na maandamano tukaamua kushuka chini kuunda uongozi kitongoji kwa kitongoji Tanzania nzima,”alisema.
Amshangaa JK kuhusu Katiba
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Ndesamburo---CCM-wataendelea-kunisindikiza--Moshi-Mjini/-/1597296/2491846/-/xq7w2yz/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Ndesamburo---CCM-wataendelea-kunisindikiza--Moshi-Mjini/-/1597296/2491846/-/xq7w2yz/-/index.html
No comments
Post a Comment