Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Thursday, October 16, 2014

Msumbiji: uchaguzi mkuu wafanyika

    
Picha za wagombea zikiwa kwenye mabango kwa ajili ya uchaguzi nchini Msumbiji.
Picha za wagombea zikiwa kwenye mabango kwa ajili ya uchaguzi nchini Msumbiji.
RFI / Alexandra Brangeon

Na RFI
Wananchi wa Msumbiji wanapiga kura leo Jumatano kumchagua rais mpya, lakini pia kuwachagua wabunge katika uchaguzi mkuu kote nchini.

Wagombea urais ni pamoja na Filipe Nyusi wa chama tawala, cha Frelimo, Alfonso Dhlakama mwaasi wa zamani wa Renamo na Daviz Simango wa chama cha MDM.
Tume ya Uchaguzi imeahidi kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki.
Uchaguzi huu ni muhimu kwa raia wa nchi hiyo ambao wanasema rais atakayechaguliwa wana imani kwamba atamaliza tofauti ambayo imekuwa ikishudiwa kati ya serikali na waasi wa zamani RENAMO.
Msumbiji ni nchi ambayo inakabiliwa na matatizo mbalimbali tangu ipate uhuru mwaka 1975, hususan ukosefu wa ajira, umasikini, uchumi umekua ukidorora siku baada ya siku,...
Baadhi ya raia wamekua wakua wakiwalaumu wanasiasa, hasa serikali kwa namana haishughulikii ajira kwa raia wake. Hayo ya kijiri baadhi ya raia ambao wameongea na RFI wamesema hawatoshiriki uchaguzi kwani hakuna faida yoyote watakayoipata, bali uchaguzi huo utawafaidi wanasiasa ambao watakua wamefaulu kushinda.
Katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Msumbiji, wanafunzi wamegawanyika katika makundi. Baadhi wanasema wanataka mabadiliko katika sekta mbalimbali, hususan ajira, uchumi pamoja na miundombinu.
“ Lakini mabadiliko yanatiya wasiwasi, kwani watu wengi hapa kusini wana wasiwasi na Renamo. Renamo iliua watu wengi wakati wa vita vilyodumu miaka 16”, amesema Abel , mmoja kati ya wanafunzi hao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment