Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, October 23, 2014

Burkina Faso yajaribu kuondoa mihula miwili ya urais .

Rais wa Burkina Faso Blaise  Compaore alipokutana na  na aliyekuwa mgombea urais wa Guinea 2010  Cellou Dalein Diallo huko Conakry Guinea.
Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore alipokutana na na aliyekuwa mgombea urais wa Guinea 2010 Cellou Dalein Diallo huko Conakry Guinea.

Serikali ya Burkina Faso inafanya msukumo mpya  kuondoa masharti ya mihula miwili ya urais wa nchi hiyo.
Waziri wa mambo ya ndani  alisema Jumanne serikali itawasilisha muswaada bungeni kuitisha kura ya maoni juu ya suala hilo.
Wafuasi wa rais wa muda mrefu Blaise Compaore wametaka mabadiliko hayo ambayo yatamruhusu kugombea tena mwaka ujao wakati muhula wake wa pili utakapomalizika.
Kiongozi wa upinzani Benewende Stanislaus Sankara amesema upinzani utapinga mapendekezo ya kura hiyo ya maoni.
 Amesema serikali ina agenda ya siri katika majaribio ya hivi karibuni ya mazungumzo na kwamba wana ushahidi kuwa wale walioko madarakani wanataka kuichezea katiba.” Alisema wanasubiri kuona ikiwa bunge litazingatia  matakwa ya wengi  au matakwa ya mtu mmoja.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment