Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, October 25, 2014

Brazil: rais wa zamani Lula ashiriki katika kampeni ya Dilma Rousseff
Rais wa zamani Lula ashiriki katika kampeni ya Dilma Rousseff. Hapa ni katika mji wa Sao Paulo, Oktoba 20 mwaka 2014.
Rais wa zamani Lula ashiriki katika kampeni ya Dilma Rousseff.

Na RFI
Duru ya pili ya uchaguzi wa rais utafanyika Jumapili Oktoba 26 nchini Brazil. Rais anayemaliza muda wake Dilma Rousseff, ambaye anagombea muhula wa pili anaendelea kupata wafuasi wengi katika kampeni anazozifanya.


Dilma Rousseff kwa sasa anamshinda alama kati ya sita na nane mpinzani wake wa chama cha PSDB, Aecio Neves. Moja ya nguvu anazopata Dilma Rousseff katika kampeni zake ni kuungwa mkono na rais wa zamani wa Brazil Lula, ambaye bado ni maarufu nchini humo.
Kampeni hizo za uchaguzi kwa duru ya pili zinaonekana kuwa na motisha ikilinganishwa na kampeni za duru ya kwanza ya uchaguzi. hayo yanajiri wakati wafuasi wa Dilma Rousseff walihasimiana Alhamisi Oktoba 23 na wafuasi wa Aecio Neves katika mji wa sao Paulo.
Rais wa zamani Lula, ambaye bado ana umaarufu mkubwa nchini Brazil, amekubali kushiriki katika kampeni ya Dilma Rousseff. Kwa mujibu wa Lula, haya ni mapambano kati ya matajiri na maskini. Maskini ambao maisha yao yameinuka katika kipindi cha miaka kumi na mbili iliyopita, tangu walipokua madarakani Wasoshalisti, amesema Lula .
" Matajiri hawapendi kuwaona maskini wakinufaika au kusafiri kwa ndege", ameongeza Lua. Katika mkutano uliyoendeshwa katika mji wa Rio, Lula amemshambuliwa kwa maneneo makali mgombea wa upinzani, Aecio Neves, ambaye alimuita "playboy" na "mtoto wa baba." akimfananisha na mtu ambaye hana haja ya kitu. "
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment