Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, September 23, 2014

ZIARA YA KINANA JIMBO LA CHALINZE YAMNUFAISHA MLEMAVU
 Polisi na Kijana Hamis Gabriel (kushoto)  wakimsaidia Mama mwenye ulemavu Halima Salehe, aliyefika kwa nia ya kumuona Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwenye uzinduzi wa soko jipya la kisasa la Mbwewe, katika jimbo la Chalinze, Kinana akipofika kwenye soko hilo akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza uterkelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Pwani, Septemba 22, 2014. Baadaye Kinana alimuona na kumpa mama huyo msaada wa sh. 200,000.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiingia kwenye jengo la Kituo cha Polisi Mbwewe kuzindua ujenzi wa kituo hicho leo, Septemba 22, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo la Chalinze  mkoa wa Pwani.
 Jengo la zamani la Kituo kidogo cha Polisi Mbwewe.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba 22, 2014 kwenye Uwanja wa Ofisi za Kata ya Miono, jimbo la Chalinze, akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM mkoa wa Pwani. Nyuma yake ni Katibu wa NEC, Itukadi na uenezi, Nape Nnauye.
 Wasanii wakionyesha umahiri wao wa kucheza ngoma katika mkutano wa Kinana uliofanyika Miono, jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) "akimsimamia' Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, wakati akichapia jengo la Kituo cha Polisi Miono, jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani.
 Katibu Mkuu wa CCM Kinana akichapia kushiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi Miono
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofsi ya CCM Kaya  ya Kiwangwa, jimbo la Chalinze. Pembeni yake ni Kinana akishuhudia
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment