Wadau, ni matumaini yangu kuwa hamjambo na Mwenyezi Mungu, Muumba Mbingu na Ardhi, Muweza wa kila kitu amewaamsha salama. Kwa wale ambao leo ni wagonjwa tunawaombee kwa Mungu wapone mapema ili waendelee na majukumu yao ya kila siku. Kwa wale ambao hawakubahatika kuiona siku ya leo, tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu ili awalaze mahala pema Peponi. Ameen.

Wadau, leo Jumatano tarehe 24 Septemba 2014 ni siku muhimu sana katika historia ya nchi yetu na ya Bunge Maalum la Katiba ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge atawasilisha Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya. Hii ni baada ya Chenge kuwasilisha jana rasimu hiyo kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Sammuel Sitta. Wakati akikabidhi rasimu hiyo, Chenge alisema kuwa kazi ya kuchambua taarifa za kamati zote 12 ili kupata rasimu hiyo ilikuwa ngumu sana. Hata hivyo, aliwashukuru wajumbe wa Kamati yake kwa kazi nzuri waliyofanya ambapo wakati mwingine walilazimika kufanya kazi hadi usiku wa manane.

Kama kawaida ya JF, tutakuwa hewani moja kwa moja kutoka Bungeni Dodoma ambapo tutawaletea yatakayojiri wakati wa uwasilishaji wa Rasimu hiyo. Tutawaletea dondoo za mambo muhimu ambayo yatawasilishwa na Chenge.

Pamoja nami, nitakuwa na wadau kadhaa ambao tumekuwa tukiwaletea yanayojiri Bungeni tangu vikao vya Bunge Maalum vilipoanza. Hadi wakati huo, Stay Connected

****************************UP DATES*************************


*Sasa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge anaanza kuwasilisha.mtuwe pamoja.


*Chenge anaanza kwa salamu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anasema kuwa taarifa iliyowasilishwa kwa Mwenyekiti na hatimaye mbele ya bunge maalum inawasilishwa kwa mujibu wa kanuni ya 35 kanuni ndogo ya 9. Anasema kuwa Rasimu ina kurasa 350 ambayo hataweza kuisoma yote na badala yake kamati imeandaa muhtasari ambao atauwasilisha


*Chenge Anatoa shukrani kwa kuruhusu mchakato wa katiba mpya. Anaishukuru pia tume ya mabadiliko ya katiba kwa kazi nzuri ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi ambayo ndiyo msingi mkuu wa mijadala ya bunge maalum la katiba. Anamshukuru pia Mwenyekiti Sitta kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi. Anasema kuwa uteuzi huo umemfanya awe sehemu ya historia ya nchi hii katika kuandika katiba mpya. Pia anamshukuru Makamu Mwenyekiti, kwa usimamizi mzuri. Pia anawwpongeza wajumbe wa kamati zote kwa kazi kubwa waliyofanya


*Anasema kuwa ka mujibu wa kanuni ya 35, fasili ndogo ya saba, tarehe 15 Septemba 2014, kamati ya uandishi ilipew kazi yamkuandaa Rasimu ya Katiba. Anasema kuwa waliongozwa na mambo matatu katika kufanikisha kazi hiyo ambayo ni
Maoni ya Walio wengi, walio wachache na mjadala bungeni
kuangalia katiba za nchi nyingine
kuangalia misingi ya uandishi wa Katiba


*Anasema kuwa ka mujibu wa kanuni ya 35, fasili ndogo ya saba, tarehe 15 Septemba 2014, kamati ya uandishi ilipew kazi yamkuandaa Rasimu ya Katiba. Anasema kuwa waliongozwa na mambo matatu katika kufanikisha kazi hiyo ambayo ni
Maoni ya Walio wengi, walio wachache na mjadala bungeni
kuangalia katiba za nchi nyingine
kuangalia misingi ya uandishi wa Katiba


*Anaainisha mambo ambayo wabunge wengi waliyakadili ikiwa ni pamoja na muundo wa muungano, uwiano wa kijinsia, mamlaka ya Rais wa Zanzibar, Mamlaka ya Zanzibar Kukopa, Nafasi ya Rais wa Zanzibar katika serikali ya muungano, serikali za mitaaa, haki za vijana, wazee, watoto, wakulima, wavuvi, wafugaji, wachimbaji wadogo, malengo muhimu ya uchumi, ukomo wa wabunge, TAKUKURU kuingizwa kwenye katiba, madaraka ya Rais, nk


*Anasema kuwa katiba ya nchi ni sheria mama ya nchi yoyote. Hivyo anasema kuwa wameandika katiba ili kuondoma uwezekano wa kufanya marekebisho ya mara kwa mara. Hivyo anasema kuwa katiba imeainisha masharti ya kufanya marekebisho ambayo ni theluthi mbili ya wabunge toka Zanzibar na Theluthi Mbili kutoka Tanzania bara


SURA ZA RASIMU YA KATIBA


SURA YAMKWANZA
*Anasema kuwa Rasimu ya Warioba imebendekeza muundo wa serikali tatu. Hata hivyo licha ya wachache kupendekeza muundo huo uendelee, wajumbe walio wengi walipendekeza kufutwa kwa muundo wa shirikisho kutokana na sababu zifuatazo;
Hati ya Muungano ambayo ndiyo msingi mkuu wa muundo wa muungano haikuanzisha muundo wa shirikisho wa serikali tatu
Mapendekezo ya kuanzisha muundo wa muungano yanapingana na Sheria ya Mabadilikomya Katiba
Muundo wa shirikisho utasababisha mgawanyiko miongoni mwa jamii katika pande zote za muungano ambao umedumu kwa zaidi ya nusu karne
Utatuzi wa kero za muungano hautegemei wingi na idadi ya serikali bali dhamira ya tatu katika kutatua kero hizo


SURA YAMKWANZA
*Anasema kuwa Rasimu ya Warioba imebendekeza muundo wa serikali tatu. Hata hivyo licha ya wachache kupendekeza muundo huo uendelee, wajumbe walio wengi walipendekeza kufutwa kwa muundo wa shirikisho kutokana na sababu zifuatazo;
Hati ya Muungano ambayo ndiyo msingi mkuu wa muundo wa muungano haikuanzisha muundo wa shirikisho wa serikali tatu
*Mapendekezo ya kuanzisha muundo wa muungano yanapingana na Sheria ya Mabadilikomya Katiba
Muundo wa shirikisho utasababisha mgawanyiko miongoni mwa jamii katika pande zote za muungano ambao umedumu kwa zaidi ya nusu karne
Utatuzi wa kero za muungano hautegemei wingi na idadi ya serikali bali dhamira ya tatu katika kutatua kero hizo


*Kutokana na maoni hayo ya wananchi, Kamati ya Uandishi imefanya marekebisho ya Ibara hiyo na kurudisha muundo wa muungano wa serikali mbili


*Rais wa Jamhuri amepewa mamlaka ya kugawa mikoa na wilaya kwa Tanzania Bara na amekasimu madaraka ya kugawa mikoa na wilaya kwa Zanzibar


TUNU ZA TAIFA
Chenge anataja Tunu 4 zilizokubalika na ambazo zimo kwenye Rasimu ya Tatu ambazo ni;
Lugha ya Kiswahili
Muungano
Utu na udugu
Amanimna Utulivu




MISINGI YA UTAWALA BORA
Uwazi
uwajibikaji
Demokrasia
utawala wa kisheria
haki za binadamu
usawa wajinsia
uzalendo


SURA YA PILI


MALENGO YA TAIFA
Malengo Makuu kwa Ujumla
kisiasa
kijamiii na kiutamaduni
Utafiti, dira ya kiuchumi nk
Sera ya mambo ya nje


MALENGO YA KIUCHUMI, KIJAMII NA KIUTAMADUNI
kujenga uchumi wa kisasa kwa kuhimiza mapinduzi katika kilimo, uvuvi na ufugaji. Pia kuhakikisha nishati ya gesi inapewa kipaumbele.
- kujenga vyuo vvya kiufundi
-kuimarisha vyama vya ushirika
- Kujenga utaratibu wa kujenga viwanda vidogo na vya kati ili kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na madini
-Umiliki ardhi,
-Kuhamasisha uwekezaji wa pamoja baina ya raia na wasio raia
- kuweka mazingira ya kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote na maendeleo linganifu


LENGO LA KATIBA KIJAMII
-Kuhifadhi heshima ya binadamu kwa kufuata mikataba na haki za kimataifa
-vyombo vya umma vinatoa haki sawa kwa watu wote
-huduma za kijamii zinatolewa kwa wazee, watoto na waru wasiojiweza
-huduma za uwakili kwa watu wasiojiweza
-haki ya elimu kwa fani ,tu anayoipenda na hivyo kujiendeleza hadi upeo wake
-haki ya afya na uzazi salama


SURA YA TATU


ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA


-kwa kuwa suala la Adhi si la muungano, kamati inapendekeza kuweka misingi ya matumizi ya rasilimali zilizopo ndani ya Ardhi. Pia kwa kuwa Tanzania bara hakuna Katiba, ni vema misingi ikawekwa ili kukwepa kuingiliana na Serikali ya Zanzibar katika jambo hili. Chenge anasema kuwa sura hii ni mpya na haikuwemo kwenye Rasimu ya Warioba. Rasimu inaeleza misingi ya umiliki na matumizi ya ardhi, maliasili na mazingira

****************************** **UPDATES********************* ****
*Watumishi wa umma hawataruhusiwa kugombea uongozi ndani ya chama cha siasa
*Uraia pacha umekataliwa isipokuwa watapewa hadhi maalum hasa katika masuala ya kiuchumi. Hawataruhusiwa kuchagua au kuchaguliwa kisiasa
* Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
*Mgombea Mwenza ataendelea kuwepo kwenye katiba mpya.

BUNGE
*Mawaziri kuendelea kuwa Wabunge
*Waziri Mkuu kuendelea kutambulika ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
*Kuna Ibara zinazohusu serikali za mitaa tofauti na Katiba ya Warioba ambayo haikuwa na ibara hiyo
*Muundo uliopo wa Bunge uendelee. Yaani Bunge litakuwa na sehemu mbili ambayo ni Rais na wabunge
*kutakuwa na wabunge wa aina tano ambao ni Wa kuchaguliwa, Walemavu watano, wabunge 10 wa kuchaguliwa na Rais, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Spika kama hatokani na wabunge
*Kuhusu Ukomo Juu wa Idadi ya Wabunge ni 360. Hapo wamezingatia uwiano wa wanawake na wanaume na ukubwa wa ukumbi
*Maisha ya Bunge yatakuwa ni muda usiozidi miaka 5 yaani kuanzia Bunge la kwanza linapoitishwa baada ya uchaguzi hadi uchaguzi Mkuu Mwingine
*Sifa ya kuwa mbunge nimkujua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au kiingereza
*Kutakuwa na mgombea huru ambapo wananchi wasio wafuasi wa vyama vya siasa kugombea nafasi za ubunge. Hata hivyo kutakuwa na katazo kwa mbunge aliyegombea akiwa huru kujiunga na chama cha siasa. Kwamba atapoteza ubunge wake endapo atajiunga na chama cha siasa awapo madarakani.
*Ukomo wa ubunge kama ilivyo kwenye rasimu ya Warioba umeondolewa hivyo kwa Rasimu ya Tatu haijatoa ukomo wa ubunge
* Haki ya wananchi kumuondoa madarakani mbunge kabla ya muda wake kama ilivyotolewa na Rasimu ya Warioba imeondolewa na sasa wananchi watamwajibisha mbunge baada ya miaka 5 endapo hawakuridhishwa na utendaji wake.
*Kuhusu Spika na Naibu Spika kutotokana na Wabunge au vyama vya siasa, kamati zote 12 zimependekeza kuwa anaweza kutokana na wabunge. Hata hivyo Rasimu ya Tatu imeweka ulazima kwa Spika kutokana na Wabunge.
*Kutakuwa na baraza la wawakilishi wa Zanzibar

MAHAKAMA*Kutakuwa na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
* Kutakuwa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufaa
*Mahakama ya juu ndiyo itakayokuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri ya Kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais
*Kutakuwa na Mahakama kuu ya Tanzania Bara na Mahakama Kuu ya Tanzania Zanzibar. Mahakama hizi zitakuwa na hadhi sawa
*Mahakama ya Kadhi na Maamuzi ya chombo hicho itatambuliwa ndani ya katiba na kwenye sheria za nchi

UCHAGUZI NGAZI YA KITAIFA*Kutakuwa na mgombea huru kwa Nafasi ya Rais na Mbunge. Hata hivyo, bunge litatunga sheria kuhusu idadi ya wapiga kura watakaomdhamini, kipindi cha kukoma uanachama wa chama cha siasa kabla ya uchaguzi, kumzuia kujiunga na chama cha siasa akiwa madarakani, kueleza chanzo cha mapato, aandae ilani ya uchaguzi, asiwe na muelekeo wa kuligawa taifa

TAASISI ZA UWAJIBIKAJIkutakuwa na taasisi zifuatazo
*Tume ya Utumishi na Maadili ya Umma
*Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu z Serikali