Writen by
sadataley
6:53 AM
-
0
Comments
VIONGOZI WA DINI NA WAZEE KALENGA WASIFU UTENDAJI WA MBUNGE MGIMWA ,MWENYEWE AWACHANGIA MILIONI 4.5
Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi (Ihemi) la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Mchungaji Aikam Chavalla akimshukuru mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya Jimbo la Kalenga
VIONGOZI wa dini na wazee katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa wameeleza kufurahishwa na utemndaji kazi wa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa na kuwa wao kama viongozi wa dini kazi yao kubwa ni kuendelea kumwombea ili azidi zaidi ili kuendelea kuwatumikia wananchi wa Kalenga. Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana jumapili baada ya mbunge huyo kufanya ziara katika makanisa mawili ya kata ya Ifunda likiwemo Kanisa la Romani cathoric (RC) parokia ya Ifunda na kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Ifunda kibaoni viongozi hao walisema wamepata kuwa na wabunge zaidi ya wanne katika jimbo hilo ila utendaji wa Mbunge umekuwa na matumaini makubwa kiasi cha wananchi kujivunia uwajibikaji wa mbunge wao. Mkuu wa jimbo la kusini Mashariki Ihemi katika kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa mchungaji Aikam Chavalla alisema kuwa kwa zamani jimbo hilo ilikuwa ni vigumu kwa mbunge kuitwa kwa dharula kanisani na kufika kushiriki na wapiga kura wake . Pia alisema wao kama viongozi wa dini wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na viongozi mbali mbali wa serikali hasa ukizingatia kuwa wote ni viongozi ila kila mmoja anamtegemea mwenzake katika kuongoza na kuwa wakati viongozi wa serikali na wabunge wanawakilisha watu katika utawala wa umma na wao viongozi wa dini wapo kwa ajili ya kuwaombea wote kufika katika ufalme wa mbinguni. Hivyo alisema kuwa jimbo la Kalenga litaendelea kuwa na maendeleo iwapo viongozi wote wataiga mfano wa mbunge Mgimwa katika kuwatumikia wananchi badala ya wabunge wengine ambao walikuwepo kwa ajili yao pekee. Kwa upande wake paroko wa kanisa la RC Ifunda Alois Mdemu alisema kuwa mchango wa kiongozi huyo katika maendeleo unafanana na ule wa marehemu babake mbunge aliyefariki Dr Wiliam Mgimwa ambae pia alikuwa akijitoa zaidi kwa ajili ya wananchi wake. Paroko Mdemu alisema kuwa mbali ya kuwa Godfrey Mgimwa ni mbunge kijana ila kazi anayoifanya inaonyesha si kijana tena bali ni baba wa wananchi wote wa Kalenga na hivyo iwapo ataendelea hivyo wana kalenga kamwe hawatajisikia yatima kwa kuondokewa na mbunge wao Dr Mgimwa. Mbali ya viongozi hao wa dini pia wazee wa kata ya Ifunda wamesema kuwa kutokana na utendaji wa mbunge huyo hadi sasa hawahitaji mbunge mwingine zaidi ya Mgimwa katika jimbo hilo ila hawawazuii wanaofika kuchangia maendeleo ya jimbo hilo kuunga mkono wa mbunge wao Mgimwa. Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake mwenyekiti wa kikundi cha Vicoba cha wazee Ifunda BEatus Mduda alisema kuwa uanzishwaji wa kikundi hicho umechangiwa kwa kiasi kikubwa na mbunge huyo na kuwa toka nchi ipate uhuru jimbo la kalenga halijapata kuwa na mbunge ambae amewakumbuka wazee kama Mgimwa na kuwa wao kama wazee hawaoni sababu ya kuwa na mbunge zaidi yake tena . "Tunatambua umri wako bado kijana hivyo hata tukiendelea kukuchagua kwa vipindi zaidi ya vinne bado nguvu ya kututumikia wananchi wa Kalenga unayo hivyo sisi wazee tayari tumeanza kuwashawishi vijana wetu kuwapuuza wale wote wanaojipitisha jimboni kutaka ubunge na tunaomba CCM kuwashughulikia wote wanaofanya kampeni za ubunge" Mbunge Mgimwa alisema kuwa katika ziara yake hiyo ndani ya kata ya Ifunda na kijiji kimoja hicho cha ifunda kibaoni amechangia kiasi cha Tsh milioni 4.5 kwa ajili ya kwaya ya Mtakatifu Secilia katika kanisa la RC kiasi cha Tsh milioni 2 ,mchango kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya muziki kanisa la KKKT Ifunda kiasi cha Tsh milioni 1 na mchango kwa ajili ya uanzishwaji wa vicoba kwa kikundi hicho cha wazee kiasi cha Tsh milioni 1 na kuwa ataendelea kufanya hivyo kwa wananchi wake wa kata na vijiji vyote iwapo watamshirikisha.
Habari kwa hisani ya www.matukiodaima.co.tz
|
No comments
Post a Comment