Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, September 24, 2014

Rais Kikwete akabidhiwa zawadi na Watanzania wa Marekani        
Rais Kikwete awahutubia watanzania katika hafla ya "Usiku wa Jakaya", Washington DC
Rais Kikwete awahutubia watanzania katika hafla ya "Usiku wa Jakaya", Washington DC
               
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, amesema ukuwaji wa haraka wa uchumi wa nchi za Afrika haujaweza kuwanufaisha wananchi walo wengi kwa sababu ukuwaji wa sekta ya kilimo ambayo wananchi wengi wanategemea haijakua kwa haraka.
 
Rais wa Tanzania Kikwete akizungumza kwenye jopo juu ya kupambana na umaskini uloandaliwa na USAID
Rais wa Tanzania Kikwete akizungumza kwenye jopo juu ya kupambana na umaskini uloandaliwa na USAID

Akizungumza katika jopo la wataalamu wa kimataifa lililotayarishwa na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani, USAID, hapa Washington siku ya Ijuma Rais Kikwete anasema, ingawa ripoti mpya ya Benki Kuu ya Dunia juu ya "Kukomesha ufukara ulokithiri na kuhamasisha ukuwaji" inaeleza kwamba ufukara duniani umepunguka kwa kasi mnamo miongo mitatu iliyopita, lakini anasisitiza kwamba wananchi wa Afrika hawajashuhudia mabadiliko hayo ya haraka.
Kiongozi huyo wa Tanzania, aliyewasili Marekani kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Umoja wa Mataifa anasema mengi yanahitajika kufanywa ili kuweza kubadili hali hiyo kwa kuwekeza zaidi katika kilimo.
Na katika hafla nyingine iliyoandaliwa na Watanzania wanaoishi Marekani pamoja na wanachama wa chama tawala cha Tanzania cha CCM, Rais Kikwete, alieleza furaha yake kutokana na kwamba pendekezo lake la kuwataka Watanzania, hapa Marekani kuungana na kuunda vikao vya mashauriano na kusaidiana limetekelezwa kupita alivyo tarajia.
"Usiku wa Jakaya" ni hafla iliyoandaliwa hasa na wanachama wa CCM ili kumpongeza kiongozi wao kutokana na mafanikio aliyoyafanya mnamo miaka 10 ya utawala wake wa awamu ya nne Tanzania.
Rais Kikwete anashanga na ukubwa wa kombe alokabidhiwa na wajumbe wa CaliforniaRais Kikwete anashanga na ukubwa wa kombe alokabidhiwa na wajumbe wa California
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment