Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, September 18, 2014

Marekani kupeleka wanajeshi Afrika magharibi kupambana na Ebola

Mataifa yaliokumbwa na Ebola katika Afrika magharibi, Agosti 30, 2014
Mataifa yaliokumbwa na Ebola katika Afrika magharibi, Agosti 30, 2014
               
Rais Barack Obama atatangaza juhudi za Marekani za kusaidia nchi za Afrika Magharibi kupambana na ugonjwa hatari wa Ebola.  Bwana Obama atatangaza mpango wa kupeleka wanajeshi 3,000 huko Afrika Magharibi  Jumanne jioni akiwa katika taasisi ya kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Marekani-CDC mjini Atlanta , Georgia.
Wanajeshi hao watajenga vituo 17 vya afya na  kila kituo kitakuwa na  vitanda 100  ili kuweza kuwatenga na kutibu walioambukizwa  kirusi  cha ugonjwa wa Ebola.
Ujumbe huo wa Marekani pia utajenga kituo cha kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya 500 kwa wiki. Kwa mujibu wa taarifa kutoka White House kituo cha usimamizi wa  shughuli hiyo kitakuwa  katika mji mkuu  wa Liberia, Monrovia.
Wakati huo huo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litafanya kikao cha dharura Alhamis kuzungumzia ugonjwa huo. Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa, Samantha Power alisema ugonjwa huo ni hatari kwa jumuiya ya kimataifa na ni lazima dunia ishirikishwe kupambana nao.
Valerie Amos
Valerie Amos
Nao maafisa wa shirika la afya Duniani-WHO walisema mataifa ya magharibi yaliyokumbwa na ugonjwa wa Ebola yako katika ukingo wa mgogoro mkubwa wa kibinadamu kama hayatapatiwa msaada karibuni.
Mratibu wa misaada ya dharura katika WHO, Valerie Amos alisema akiwa huko Geneva kuwa nchi ya Liberia na Sierra Leone bado zinajaribu kujikwamua kutokana na migogoro ya kibinadamu iliyotokea chini ya muongo mmoja uliopita na nchi ya Guinea ndio kwanza inajikwamua kutoka katika mgogoro wa kisiasa.
Chanzo : voa swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment