Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, September 18, 2014

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA MAFIA, AREJEA NYAMISATI KWA USAFIRI WA MASHAKA WA BOTI YA KIZAMANI
 Katibu Mkuu wa CCM, akipanda boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari kutoka Kisiwa cha Mafia kwenda Nyamisati wilayani Rufiji, baada ya kumaliza ziara yake katika wilaya ya Kisiwa hicho, leo Septemba 17, 2014, akiwa katika ziara ya mkoa wa Pwani, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoahuo. Boti hiyo ambayo pia hutumiwa na wananchi kusafiria kati ya kisiwa hicho cha Mafia na Nyamisati Kinana amesafiri nayo kwa saa nne tangu saa sita mchana hadi saa 11 jioni.
 Katibu Mkuu wa CCM akipanda boti hiyo kwa ukakamavu
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye boti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza, ambaye aliwasili wilayani Mafia kwa ndege lakini akalazimika kusafiri na Kinana kwa boti hiyo kurejea Nyamisati. Watatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao.
 Katibu wa NEC, Itikadina Uenezi, Nape Nnauye (watatu kushoto), akiwa kwenye boti na abiria wengine waliosafiri pamoja na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
 Baadhi ya maofisa wa CCM na Waandishi wa habari wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Umma wa Makao Makuu ya CCM, Daniel Chongolo (watatu kushoto) akiwa na abiria wenzake katika boti hiyo kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
 Abiria wengine wakiwa katika boti hiyo kutoka Mafia kwenda Nyamisati leo. Kushoto ni Mwandishi wa Clouds TV/Radio Salum Mwinyimkuu.
 Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
  Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mama Salma Kikwete ya Wama iliyopo wilayani Rufiji, baada ya kutoka Mafia. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Suma Mesa. Kinana amempongeza Mama Salma kwa uamuzi wake wa kuanzisha shule hiyo ambayo ni maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa watoto yatima kutokamikoa mbalimbali nchini.
 Watoto wa shule hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu Kinana.
Kinana akiondoka kwenye shule hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao na watatu kushoto ni Mwandishi wa habari wa gazeti la Jamboleo, Saidi Mwinshehe na kulia ni Chongolo. Kinana anatarajiwa kuendele na ziara yake katika mkoa wa Pwani kesho, Septemba 18, 2014. Maelezo/Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment