Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, September 24, 2014

KATIBA MPYA: Bunge kutuma ofisa Saudia kusimamia kura


Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba, Andrew Chenge akionyesha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo, mjini Dodoma jana. Rasimu hiyo inatarajiwa kuwasilishwa bungeni leo. Picha na Owen Mwandumbya 
Na Daniel Mjema na Sharon Sauwa, Mwananchi
 
Dodoma. Ofisi ya Bunge la Katiba itamtuma ofisa wake kwenda Makka, Saudi Arabia kusimamia upigaji kura kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa wajumbe wa Bunge hilo wanaokwenda Hijja.

Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alipotakiwa kueleza idadi kamili ya wajumbe wa Bunge hilo wanaotarajiwa kuwa nje ya nchi na jinsi watakavyopiga kura.

Juzi, Bunge hilo lilizifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwaruhusu wajumbe watakaokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge wakiwamo wanaokwenda Hijja kuipigia kura Katiba inayopendekezwa, iliyokabidhiwa kwa Kamati ya Uongozi jana.

Chini ya marekebisho hayo, mjumbe aliye nje ya Bunge, ataruhusiwa kupiga kura ya wazi au ya siri kwa njia ya fax au mtandao kama itakavyoelekezwa na katibu kwa kushauriana na mwenyekiti.

Hamad alisema hadi kufikia jana mchana walikuwa wamewatambua wajumbe wanane ambao watakwenda Hijja huko Uarabuni lakini orodha ya watakaokuwa nchi nyingine bado haijajulikana.
Hamadi alisema ofisa wake huyo atasimamia kura za wajumbe wanaokwenda Hijja katika upigaji kura unaotarajiwa kuanza Septemba 29 hadi Oktoba 2 mwaka huu.

Alisema ni vigumu kutaja vituo watakavyopigia kura sasa kwa sababu bado hawajawauliza wajumbe wengine waliopo nje ya nchi ambao wangependa kupiga kura wakiwa huko.

Kuhusu iwapo watapiga moja kwa moja kwa mtandao au watapiga kwenye karatasi na kutoa vivuli, Hamad alisema suala hilo litaamuliwa na Kamati ya Uongozi ya Bunge chini ya Mwenyekiti, Samuel Sitta.

Ukawa wapinga
Wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba na James Mbatia wamelishukia Bunge hilo kwa kuruhusu upigaji kura nje ya nchi.

Akizungumza jana, Profesa Lipumba alisema kilichofanywa na Sitta na wajumbe wake ni uchakachuaji unaoweza kuliingiza Taifa kwenye mgogoro mkubwa.

“Kwanza taratibu za kura mabunge ya Jumuiya ya Madola ni kura zote zinapigwa ndani ya Bunge. Unapozungumzia akidi imetimia ni wajumbe walioko ndani ya Bunge,” alisema Profesa Lipumba.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/KATIBA-MPYA--Bunge-kutuma-ofisa-Saudia-kusimamia-kura/-/1597296/2463400/-/dcjkfg/-/index.html
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment