Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, September 26, 2014

Ibara 28 za Tume ya Warioba zilizoondolewa


Jaji Warioba.PICHA|MAKTABA 
Na Sharon Sauwa na Julius Mathias, Mwananchi
Dar/Dodoma. Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iliyowasilishwa bungeni juzi, imeondoa Ibara 28 zikiwamo zinazowataka viongozi wa umma kutopokea zawadi kwa manufaa yao binafsi wala kufungua akaunti ya benki nje ya nchi pasipo sababu maalumu, Mwananchi limebaini.

Ibara ya 15 iliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ilisema: “Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ilitaka Bunge kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano. Mbali na ibara hiyo, pia Ibara ya 16 iliyohusu ufunguaji akaunti nje ya nchi, imeondolewa.

Ibara nyingine zilizoondolewa ni pamoja na ya 17 iliyopendekeza uwazi wa mali ikimtaka kiongozi wa umma kutangaza thamani ya mali na madeni yake mara tu baada ya kupata uongozi.
Pia Ibara ya 129 iliyokuwa inawaruhusu wananchi kumvua madaraka mbunge ambaye atashindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapigakura wake au ataacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la jimbo la uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi imeondolewa.
Ibara 28 zilizoondolewa

15. (1) Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa katibu mkuu wa wizara au kiongozi wa taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:

(a) aina ya zawadi; (b) thamani ya zawadi; (c) sababu ya kupewa zawadi; na (d) mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.
(2) Neno “zawadi” kama lilivyotumika katika ibara hii linajumuisha kitu chochote chenye thamani atakachopewa kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuli za umma.

(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.

16. Kiongozi wa umma-

(a) Hatafungua au kumiliki akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna ambayo sheria za nchi zinaruhusu; na (b) hataomba au kupokea mkopo au faida yoyote kwa namna au mazingira ambayo yanashusha hadhi au heshima ya utumishi wa umma.

17.-(1) Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi, mali na thamani yake na madeni yake katika Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Ibara-28-za-Jaji-Warioba-zilizonyofolewa-zatajwa/-/1597296/2465542/-/3r28t7/-/index.html
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment