Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, September 19, 2014

DAYOSISI YA ZIWA TANGANYIKA YATARAJIWA KUFANYA MAMBO.
Zaidi ya miaka Thelathini sasa, kazi ya Wamisionari yapiga hatua mpya ya kuanzisha Dayosisi ya Ziwa Tanganyika ya Kanisa la Kiinjili Tanzania. Chimbuko la Dayosisi hiyo imetokana Misioni ya Rukwa ambayo ilikuwa inatoa huduma ya Kiroho kwa mikoa ya Rukwa na Katavi. Karibu Mwana wa Mungu tufuatane Na;Franco Nkyandwale kutoka Sumbawanga,tuone baadhi ya mambo yalivyokuwa siku ya kuwekwa kwa jiwe la Msingi la Kanisa la Usharika wa Sumbawanga Mjini. Hali hiyo iliambatanana na uchangiaji wa hali na mali ili kukamilisha Kanisa hilo baada ya miaka kumi kwa gharama ya Shilingi Bilioni 2.2 Kwa mpango wa Mungu Kanisa hilo litakapokamilika litakuwa na sura kama kifani hichooo! Askofu mteule wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika Ambele Mwaipopo alitangazwa na kikosi kazi kinachoanza kazi mara moja kama alivyoeleza Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu, Dr. Alex Malasusa. Aliyeinamisha kichwa mwanzoni kati ya picha hizo ni Mchungaji Zebedayo Mbilinyi akifahamishwa mbele ya makutano kuwa amefanya kazi kubwa ya kuiongoza Misioni ya Rukwa akiwa Mwenyekiti wa Misioni ya Rukwa na katika mchakato wa kuiendesha Dayosisi ya Ziwa Tanganyika yeye hatakuwa na majukumu makubwa isipokuwa atapangiwa kazi za kawaida. Mkuu wa Kanisa alifafanua. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimpa mkono wa pongezi Akofu Msaidizi wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika David Masaoe. Aliyesimama ni Mh. Jaji Mfawidhi Kakusulo Mwakipome Sambo wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga akitoa neno la shukrani kwa kuanzishwa Dayosisi hiyo. Wakristo waliohudhuria ibada hiyo ya kipekee Mkoani Rukwa wakiwa makini wakisikiliza mahubiri yaliyoongozwa na na Mkuu wa Kanisa. Pichani mwenye shati la michirizi na miwani ndiye Mhandisi ambaye amebuni na kuchora ramani ya Kanisa na ni Msimamizi Mkuu wa kanisa hilo na Mtaalam Mhandisi Fulgence Kibiki Masanifu Mkuu wa jengo hilo. Wakati wa mahubiri mambo yalikuwa hivi; Toa Ndugu, toa ndugu, ulichonacho Mungu, anakuona mpaka moyoni mwako, tendo hilo lilipokuwa likiendelelea nafsi yangu iliimba kimoyomoyo wimbo uliokuwa ukiimbwa nilipokuwa Sunday School miaka ya '70 wataalamu wa imani huamini kuwa ukimtolea Mungu umewekeza na mavuno yako hayatakuwa haba, ibada hiyo iliedelea kwa mtazamo huoo! Kwaya zilipata fursa ya kuhubiri kwa njia ya uimbaji, ambapo Mkuu wa Kanisa Malasusa alitoa angalizo kuwa vikundi vya Kwaya si vikundi vya burudani bali hutoa mahubiri kwa njia ya uimbaji na hicho ni sehemu ya kipawa kwa baadhi ya ya Wakristo.Waimbaji walivamia jukwaa kwa matambo ya radha tofauti. Kwaya ya Uamsho Sumbawanga. Kwaya Angalikan Sumbawanga na Moravian kutoka Kanisa Kuu mjini. Mpango wa utendaji kazi kwa muda wa miaka kumi akabidhiwa Mkuu wa Kanisa kuubariki Mkuu wa Kanisa Askofu Dr. Alex Malasusa Mchungaji Kiongozi wa Usharika waSumbawanga Mjini Calvin Kessy akiuukabidhi Mpango kzai. Askofu Mteule wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika Ambele Mwaipopo aikwa na baadhi ya vitabu vya Mpango wa Kazi ili aweze kuutekeleza,Mwenye joho jeupeee! Kamati ya ujenzi wa Kanisa hilo iilibarikiwa na kupewa jukumu la kuisimamia kazi kwa uaminifu Kamati hiyo inaongozwa na Mwnyekiti Shadrack Malila alimaarufu kwa jina la Ikuwo akiwa ameshika kipasa sauti akitoa ahadi ya uaminifu katika kusimamia kazi ya Mungu usharikani hapo. Baadhi ya Wachungaji wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika wakitoka ibadani siku hiyo. Pichani hapo chini mrefu ni Msaidizi wa Askofu Dr Shao wa Kanda ya Kaskani akiongozana Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi teule ya Ziwa Tanganyika David Masaoe katika msafara wa kuelekea nje. Jengo la Kanisa hilo lilivyoanza, Mwinjilisti Anicet Msangawale akipitapita kuangalia hatua za ujenzi. Hapa na pale kwa hatua nyingine iliyoofikiwa kwa sasa. Mungu awatie Nguvu, Hekima na Uvumilivu, hakika Mungu ashushe Baraka zake katika kuitimiza kazi hii. Hatua iliyofikiwa hii hapa. Dayosisi ya Ziwa Tanganyika itakuwa chini ya uangalizi wa Dayosisi ya Kaskazini,(Kilimanjaro),Dayosisi ya Kusini(Makete-Njombe) na Dayosisi ya Konde (Tukuyu-Mbeya)na matazamio ya harambee iliyofanyika ilikisiwa kupatikana shilingi 100,000,000/= lakini zilipatikana taslimu Mil.13 na ahadi ilikuwa 105 jumla Mil.118 zinatarajiwa kupatikana. Kazi hii ya picha na Maandishi imefanywa na Kuchambuliwa na Franco Nkyandwale, Kwa namna yoyote kama msomaji unataka kutumia picha hizo sharti utambullishe chanzo cha habari yako kwani tayari huu ni matandao wa habari.
Habari na http://ungejua.blogspot.com/2014/01/dayosisi-ya-ziwa-tanganyika-yatarajiwa.html
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment