Leo mchana Waziri Mkuu Pinda alikumbana na wakati mgumu pale Askofu wa KKKT dayosisi mpya ya Ziwa Tanganyika Ambikile Mwaipopo alipomwambia waziri mkuu afanye ubinadamu kuhakikisha bunge la katika linasitishwa ili maridhiano kwanza yafikiwe na pande zote zinazovutana.

Askofu Mwaipopo akiwa kamkazia macho Pinda amesema bunge la sasa halina uhalali wa kitaifa kutokana na mgawanyiko uliopo na kusababisha kisiwa chote cha Pemba kutokuwa na mwakilishi yoyote anaekubalika na kuchaguliwa na wananchi kwani wabunge wote wa pemba ni CUF na wote hawapo bungeni.

Amemuomba waziri mkuu kusaidia kutumia ubinadamu na uungwana kuhakikisha kuwa bunge linasitishwa ili muafaka na kisha wakirejea basi wajadili rasimu ya warioba ambayo ndio yenye maoni ya wananchi.

Pinda aliekuwa mgeni rasmi katika kuzindua dayosisi hii inayojumuisha mikoa ya Rukwa na Katavi akajibu hapohapo kwa kusema bunge ni halali na waliotoka ndio wakosaji.

Aidha Pinda akasema kinachojadiliwa ni rasinu ya warioba kwa kuiboresha na hivyo bunge la sasa halistahili lawama na kuwaomba viongozi wa dini wawasikilize wawakilishi wao waliopo bungeni (akina Mtetemela) kwa kuwa hawajaona mahali bunge lilipokosea hadi sasa.