Writen by
sadataley
4:38 PM
-
0
Comments
Mwenyekiti wa Hamashauri ya
Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, ametoa wito kwa nchi za Afrika
na duniani kote kushirikiana kuzuwia ugonjwa wa Ebola uliosambaa Afrika
Magharibi, usitapakae kwengineko.
Shirika la Afya Duniani, WHO, linakisia kuwa
watu kama 960 wamekufa kutokana na Ebola huko Guinea, Sierra Leone,
Liberia na Nigeria.Nkosazana Dlamini-Zuma alisema nchi za Afrika zinataraji kuunda kitengo cha pamoja kupambana na ugonjwa huo:
"Nchi za Afrika zimefikia uamauzi kuwa tunataka kuanzisha kitengo cha kudhibiti magonjwa.
Na tutafanya kazi pamoja na washirika wetu.
Marekani imekwishasema kuwa iko tayari kushirikiana nasi, lakini siyo pekee.
Lazima tushirikiane sana na WHO katika swala hili na washirika wengine walio tayari kuwa nasi"
No comments
Post a Comment