Writen by
sadataley
11 years ago
-
0
Comments
“Tutavidhibiti vizuri vimelea vya uchaguzi vinavyotaka kujipenyeza kwa
rushwa ndani ya baraza ili baadaye vije kuzaa mamluki wa kutumwa na
vyama vingine kukivuruga chama chetu,”
‘Tunasisitiza kuwa katika uchaguzi huu tutasimamia katiba ya chama na
mwongozo wa uchaguzi ili kupata viongozi wanaofaa kwa sababu vijana
ndiyo nguzo ya chama’
Heche
Na Raymond Kaminyoge na Edson Sosten, MwananchiDar es Salaam. Viongozi wote wa juu wa sasa wa
Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) hawatagombea nafasi yoyote katika
baraza hilo kutokana na umri wao kuzidi miaka 30.
Kwa mujibu wa katiba ya Bavicha, mgombea wa nafasi yoyote anatakiwa asiwe na umri wa zaidi ya miaka 30.
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche alisema jana
kuwa yeye, Katibu Mkuu wake, Deogratius Munishi na Naibu Katibu Mkuu,
Ester Daffi hawatagombea nafasi yoyote kutokana na umri walionao... “Hii
ina maana kuwa baada ya uchaguzi, tutaachia madaraka na kuendelea na
shughuli nyingine za chama.”
Alisema ili kuepuka udanganyifu hususan wa umri
miongoni mwa wagombea wengine katika nafasi mbalimbali za baraza hilo,
watahakikisha wanasimamia suala hilo kwa umakini mkubwa.
Heche alisema uchaguzi wa Bavicha katika ngazi ya
taifa utafanyika Septemba 10, mwaka huu na fomu zitaanza kutolewa
kuanzia Agosti 10 hadi 25 mwaka huu.
Alisema nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti bara na Zanzibar na katibu mkuu.
Nyingine ni naibu katibu mkuu bara na Zanzibar,
mratibu mhamasishaji taifa, mweka hazina na wajumbe watano wa
kuwakilisha kwenye baraza kuu la chama na wajumbe 20 wa kuwakilisha
vijana kwenye mkutano kuu wa chama hicho.
Rushwa
Akizungumzia suala la rushwa katika uchaguzi,
Heche alisema uongozi unaomaliza muda wake umejipanga kudhibiti vitendo
hivyo ili kuzuia wasaliti kujipenyeza.
Alisema kuna baadhi ya watu wamejipanga kutoa
rushwa ndani ya baraza hilo ili kushinda nafasi mbalimbali kwa lengo la
kuivuruga Chadema baadaye na kuidhoofisha.
Alisema chama hicho kitawawinda wagombea hao na
kuwafisha katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),
ili wachukuliwe hatua za kisheria na baadaye kufutwa uanachama.
Mwaka 2011, Bavicha ilifanya uchaguzi ambao
ulitawaliwa na mizengwe na vurugu hadi kusababisha kuenguliwa kwa baadhi
ya wagombea.
Wagombea walioenguliwa katika kinyang’anyiro hicho ni wale waliokuwa wakigombea nafasi ya uenyekiti, Bernard Saanane, Greyson Nyakarungu na Mtela Mwampamba kwa madai ya ukiukaji wa maadili.
Wagombea walioenguliwa katika kinyang’anyiro hicho ni wale waliokuwa wakigombea nafasi ya uenyekiti, Bernard Saanane, Greyson Nyakarungu na Mtela Mwampamba kwa madai ya ukiukaji wa maadili.
No comments
Post a Comment