Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, July 21, 2014

UZINDUZI WA ALBUM MPYA KIJITONYAMA LUTHERAN WAFANA

Oliver Israel akiimba ibadani wakati wa uzinduzi huo.
Waumini ndugu jamaa na marafiki waliofika katika kanisa la Kilutheri usharika wa Kijitonyama jijini Dar es salaam, walipata wasaa mzuri wa kumsifu Mungu pamoja na waimbaji mbalimbali waliofika kumsindikiza Oliver Israel mwimbaji wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambaye alikuwa akizindua kanda yake ya kwanza ya sauti.

Tendo la uzinduzi lilianza katika ibada ya kwanza na kuendelea ibada ya pili na kuhitimishwa wakati wa tamasha kubwa majira ya mchana ambalo mgeni rasmi mwalikwa alikuwa meya wa manispaa ya Ilala bwana Jerry Slaa ambaye alionyesha kufurahia tukio zima la uzinduzi wa album hiyo inayofahamika kwa jina la 'Nahitaji Kitu Gani?'.

Oliver ambaye alipendeza haswa kwa mavazi aliyokuwa amevaa alishikiana vyema na mumewe bwana Israel Mujumba ambaye pia ni mwimbaji na mpigaji wa kwaya ya Kijitonyama, alikuwa akimwitikia mkewe katika uimbaji huo akishirikiana na waimbaji wengine wa kwaya hiyo.

Chini ni baadhi ya picha za uzinduzi huo.

Mheshimiwa meya wa manispaa ya Ilala Jerry Slaa akizindua CD hiyo.
Oliver akimshambulia shetani.
Ilikuwa safi kabisa.
Israel akienda sambamba na mkewe.
Kucheza nyumbani mwa Bwana raha.
Hakika alipendeza na kazi ilifanyika.
Oliver akienda sawa na waimbaji wenzake huku wapigaji wa uinjilisti wakimpa sapoti ya kutosha.

Oliver Benson wa Israel akimtukuza muumba wake.
Wakati wa tamasha mchana mambo yalikuwa safi zaidi.

Upendo Kilahiro akimtukuza Mungu katika uzinduzi huo.
Kila mmoja na nakala ya album mpya. © Onai Joseph/GK
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment