Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 10, 2014

Ugunduzi mpya kuhusu Malaria


Kulingana na uchunguzi vimelea vinavyosababisha Malaria huweza kuishi mwilini kwa uboho (bone marrow) na kuepuka kinga za mwili na hivyo basi kusababisha maradhi.
Uchunguzi huu umedhihirishwa na bwana Marti ambaye alizungumza na BBC.
Swala la vimelea hivyo kujificha kwa uboho si jambo geni, lakini kundi la wanasayansi wakiongozwa na Profesa Matthias Marti katika idara ya Afya ya umma kule Harvard, Boston, walifichua hasa ambako vimelea hivyo hujificha na kutoa maonyesho.
Uzinduzi huu una umuhimu mkubwa kwa misingi kuwa umeleta ujuzi unaohitajika sana na huweza kupelekea kuundwa kwa dawa na kinga mpya za kukabiliana na vimelea hivyo ili kuzuia maambukizi.
Kwa mujibu wa wanasayansi huko Harvard, uchunguzi huu uliochapishwa na jarida la kisayansi la Science Translational Medicine, umeongeza ujuzi wa kibayologia utakaotumika kuchunguza ugonjwa wa Malaria hata zaidi.
Vimelea vinavyosababisha Malaria huambukizwa hasa kupitia Mbu, na husababisha vifo zaidi ya nusu kila mwaka ulimwenguni.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Shirika la afya duniani, zinapendekeza kuwa Malaria ilisababisha vifo laki sita mwaka wa 2012, na takriban asilimia tisini ya vifo hivyo vilitokea Afrika.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment