Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 22, 2014

Malaysia yapokea kisanduku cha ndege ya MH 17.

Mpiganaji anayeunga mkono Russia akikabidhi kifaa cha taarifa ya ndege kutoka ndege ya Malaysia nambari 17  katika mji wa Donetsk, mashariki mwa  Ukraine, Julai 22, 2014.
Mpiganaji anayeunga mkono Russia akikabidhi kifaa cha taarifa ya ndege kutoka ndege ya Malaysia nambari 17 katika mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine, Julai 22, 2014.
Waasi wanaounga mkono Russia wamekabidhi taarifa za ndege ya Malaysia iliyoanguka  kwa  wataalam wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kisanduku  kinachohifadhi taarifa za safari za ndege.
Makabidhiano hayo yalitokea Jumatatu usiku katika mji wa mashariki wa Ukraine wa Donetsk. Yalitokea muda mfupi baada ya waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak kuzungumza kwa njia ya simu na kiongozi wa waasi Alexander Borodai.
Kanal wa Malaysia Mohamed Sakri amesema masanduku hayo yalikuwa yameharibiwa  kwa kiasi fulani lakini  bado yalikuwa katika hali nzuri.
 Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jana lilikubaliana kwa kauli moja  kuwa makundi yenye silaha yanayodhibiti eneo lililotunguliwa ndege ya Malaysia nambari 17, waruhusu wakaguzi kuingia eneo hilo bila masharti.
Baraza hilo lilishutumu vikali kitendo cha kutungua ndege hiyo na kutoa mwito uchunguzi wa kina  ufanywe na  wapelelezi wa kibinafsi kutoka jumuiya ya kimataifa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment