Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 4, 2014

JOYOUS MAJI SHINGONI YAMUOMBA MPIGA NGOMA WAKE KUBAKI KUNDINI


Siyabulela Satsha (Sabu).
Habari kutoka ndani ya kundi la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini zinadai kwamba uongozi wa kundi hilo upo kwenye mazungumzo na mpiga ngoma wao maarufu kijana Siyabulela Satsha a.k.a Sabu ili aendelee kutumika katika kundi hilo mpaka DVD ya 20.

Kuwepo kwa mazungumzo hayo kulithibitishwa na Sabu mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya kuulizwa na mashabiki wake kwamba alishatangaza kuachana na Joyous imekuwaje hata baada ya kuitwa kurekodi album ya 18 lakini mpaka leo bado yupo nao, ndipo kijana huyo akasema bado Joyous wamemtaka akao kwa muda nao kidogo ila yeye alishamalizana nao kitambo.

Sabu alimaliza mkataba na Joyous mara baada ya kurekodi toleo la 17 ambapo kundi hilo kwa usimamizi wake Sabu walifanya usaili wa mpiga ngoma mpya atakayechukua nafasi ya Sabu na kupatikana kijana Irebolaji kutoka Nigeria mwenye makazi yake nchini Afrika ya kusini, lakini hata hivyo hakutumika sana na kundi hilo katika maonyesho yake sababu ikielezwa kwamba anapoteza mwendo wa mkong'osio jambo ambalo alitakiwa asitetereke kwalo kwani ingewawia vigumu kwenye kurekodi, lakini Joyous mwishowe wakaamua kumuomba Sabu arekodi tena toleo la 18 na sasa wanafikiria kumpa mkataba mpya hadi toleo la 20 ambalo litarekodiwa mwakani mwezi disemba.

Hata hivyo kwa mujibu wa Sabu hakutaka kuweka wazi alipo kijana Irebolaji kwasasa kama bado yupo na Joyous au alishaondoka.
Habari na http://www.gospelkitaa.co.tz/
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment