Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 22, 2014

Hatimaye Rais Goodluck kukutana na wazazi


Baadhi ya wazazi ambao watoto wao walitekwa nyara
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan anatarajiwa kukutana na wazazi wa wasichana waliotekwa nyara na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Rais Jonathan amekosolewa sana kwa kukosa kuongeza jitihada katika mpongo mzima wa kuokoa wasichana hao waliotekwa nyara siku miamoja zilizopita.
Wazazi hao walijiondoa katika mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika kati yao na Rais Jonathan wiki jana wakisema kuwa wanahitaji mwazo kushauriana na familia zengine za wale ambao watoto wao walitekwa.
Rais Jonathan amesema kuwa wazazi hao walichochewa na wanaharakati ambao aliwatuhumu kwa kuingiza siasa katika swala hilo zima.
Baadhi wanamkosoa Rais Goodluck kwa kukosa kukutana na wazazi hao hadi aliposhinikizwa na Malala
Wakati hayo yakijiri watu 15,000 wametoroka makwao kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mji wa Damboa baada ya ghasia zinazosababishwa na Boko Haram kukithiri.
Maafisa wanasema zaidi ya watu 40 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na Boko Haram mjini humo Ijumaa.
Wapiganaji hao pia walishambulia vijiji vingine sita.
Kadhalika wapiganaji hao wamefanya mashambulizi mengine mjini Damboa ambako waliharibu milingoti na nyaya za stima na kuwaacha wakazi wa jimbo la Borno bila umeme kwa wiki kadhaa zilizopita.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment